📰 HABARI MPYA
Inapakia habari...

HATIMAYE! ORODHA RASMI YA WANUFAIKA WA MIKOPO YA WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI KWA WILAYA YA KALAMBO YATOLEWA – WANUFAIKA WOTE WATAKIWA KUHUDHURIA MAFUNZO MUHIMU

HATIMAYE! ORODHA RASMI YA WANUFAIKA WA MIKOPO YA WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI KWA WILAYA YA KALAMBO YATOLEWA – WANUFAIKA WOTE WATAKIWA KUHUDHURIA MAFUNZO MUHIMU

 

TAARIFA KWA UMMA

Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Kalambo, Mhe. Edefonsi Joackim Kanoni, inapenda kuwajulisha wananchi wote wa Wilaya ya Kalambo kuwa Wizara ya Mifugo na Uvuvi imekamilisha mapitio ya maombi ya mikopo yaliyowasilishwa na wananchi wa Wilaya ya Kalambo kupitia programu ya uwezeshaji wa wananchi kiuchumi.

Kutokana na mchakato huo, Wizara imetoa rasmi orodha ya wanufaika waliokidhi vigezo na kufanikiwa kupata mikopo hiyo. Wanufaika kutoka Wilaya ya Kalambo ni kama ilivyoainishwa katika orodha rasmi ya Wizara, ambayo inajumuisha:

  • Rahel John Mawela – Mradi wa Mbuzi
  • Faustina Cladio Msumeno – Mradi wa Kuku wa Mayai
  • William Isaya Moringe – Mradi wa Mbuzi
  • Mashaka Medard Jastin – Mradi wa Mfumo wa Ubaridi
  • Aibini Leonard John – Mradi wa Mbuzi
  • Britney Shadi Pandisha – Mradi wa Kuku wa Nyama
  • Sisilia Augustino Michael – Mradi wa Mbuzi

Ofisi ya Mbunge inawapongeza wanufaika wote kwa kufanikiwa kupata fursa hiyo muhimu na inawatakia mafanikio katika utekelezaji wa miradi yao.

Aidha, wanufaika wote wanatakiwa kuhudhuria mafunzo maalumu ya ujuzi na usimamizi wa miradi yatakayofanyika kuanzia tarehe 29 Julai hadi 5 Agosti, 2026 katika ngazi ya mkoa. Mafunzo hayo yataratibiwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kushirikiana na Sekretarieti za Mikoa pamoja na Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Wanufaika wote wanasisitizwa kufika kwenye mafunzo wakiwa na kitambulisho halisi cha utambulisho kwa ajili ya uhakiki na kukamilisha taratibu zote muhimu kabla ya kupokea mikopo hiyo.

Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Kalambo inatoa shukrani za dhati kwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, mawaziri, viongozi na watendaji wote wa Serikali kwa juhudi kubwa wanazoendelea kuzifanya katika kuwawezesha wananchi kiuchumi na kuwaletea maendeleo endelevu wananchi wa Wilaya ya Kalambo na Taifa kwa ujumla.

Aidha, Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Kalambo, kwa heshima na unyenyekevu mkubwa, inaendelea kuiomba Serikali ya Awamu ya Sita kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuendelea kulitafakari ombi la wavuvi wa Wilaya ya Kalambo walioomba mikopo ya vizimba vya kufugia samaki. Tunaamini Serikali yetu sikivu imekuwa mstari wa mbele katika kuwawezesha wananchi kiuchumi, hivyo tuna matumaini kuwa, kadiri rasilimali na taratibu zitakavyoruhusu, ombi hilo litapata nafasi ya kuzingatiwa. Utekelezaji wa mpango huo utachochea matumizi endelevu ya rasilimali za Ziwa Tanganyika, kuongeza uzalishaji wa samaki, kuinua kipato cha wavuvi, kufungua ajira kwa vijana na wanawake, pamoja na kuchangia ukuaji wa uchumi wa Wilaya ya Kalambo na Taifa kwa ujumla. Ofisi ya Mbunge inaendelea kuishukuru Serikali kwa juhudi kubwa inazoendelea kuzifanya katika kuwaletea wananchi maendeleo.

Mwisho, Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Kalambo inaendelea kuwaomba wananchi wote wa Wilaya ya Kalambo kuendelea kudumisha upendo, umoja na mshikamano, kuheshimu sheria za nchi na kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo ili kwa pamoja tuendelee kuijenga Kalambo yenye ustawi na maendeleo endelevu.

MAWASILIANO

Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Kalambo
Simu: 0625 850 656
Barua pepe: [email protected]
Tovuti: www.mbungekalambo.com

Imetolewa na:
Musa Frackison Mzopola
Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Kalambo


Umemaliza kusoma habari hii? Tupe maoni, mtazamo au swali lako hapa chini.

Comments

MATUKIO KWA NJIA YA PICHA

Inapakia picha...

HABARI MAARUFU

FURSA ZA MIKOPO YA VIJANA SASA HADHARANI OMBA SASA UJIKWAMUE KIUCHUMI

  Katika kutekeleza ahadi ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya kutoa shilingi bilioni 200 kwa vijana ndani ya siku 100 baada ya kuingia madarakani, Wizara ya Mifugo na Uvuvi inautangazia umma kuanza kwa Awamu ya Pili ya utoaji wa mikopo yenye masharti nafuu kwa vijana. Malengo ya mikopo hiyo ni kuwawezesha vijana kupata mitaji ya kuanzisha na kuendeleza biashara ndogo, biashara za kati na kampuni changa ili kujijengea kipato katika Sekta za Mifugo na Uvuvi. Mikopo hiyo itatolewa kwa njia ya vifaa na pembejeo za uzalishaji, ikiwemo ufugaji wa samaki kwa vizimba, ufugaji wa kuku (chotara, mayai na nyama), mbuzi, kondoo na nguruwe, pamoja na boti za kuhudumia vizimba, boti za uvuvi, zana za uvuvi, mifumo ya ubari (cold chain) katika mazao ya uvuvi, mifumo ya kulazisha vifaranga vya samaki, mifumo na vifaa vya uchakataji wa mazao ya uvuvi ikijumuisha makausho ya dagaa na mwani (dryers). Vigezo na maelekezo kwa waombaji ni kama ifuatavyo: i. Baru...

NAFASI 200 ZA AJIRA ZA MAFUNDI ZATANGAZWA KWA KAZI NCHINI SAUDI ARABIA

  Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, kwa kushirikiana na Atilis Investment Limited , inawataarifu Watanzania wenye sifa stahiki kuhusu nafasi 200 za ajira za mafundi katika sekta ya ujenzi , zilizotolewa na kampuni ya Shade Corporation Limited ya nchini Saudi Arabia. KADA ZINAZOHITAJIKA Nafasi hizo zinahusisha mafundi wa kada mbalimbali, wakiwemo: Mafundi Uashi Mafundi Useremala Wasuka Nondo SIFA ZA MWOMBAJI Mwombaji anatakiwa kuwa na: Elimu ya astashahada kutoka chuo cha ufundi kinachotambuliwa na Serikali; Uzoefu wa kazi wa miaka miwili (2) au zaidi katika sekta ya ufundi; Uwezo na uzoefu katika kada husika, ikiwemo Uashi, Useremala au Usuka Nondo; Umri kati ya miaka 21 hadi 40 ; Waombaji wa nafasi hizi wanatakiwa kuwa wanaume . MASHARTI NA MAFANO YA AJIRA Waombaji watakaofaulu mchakato wa ajira watapata fursa ya kufanya kazi nchini Saudi Arabia kwa masharti yaliyowekwa na mwajiri. Miongoni mwa mafao na masharti ya ajira ni: Mshahara wa Riyal 1...

MHE. MBUNGE KANONI ASHIRIKI MAZISHI YA WAATHIRIKA WA AJALI KAZILA, ATOA WITO WA UPENDO, UMOJA NA MSHIKAMANO

  KALAMBO: Mbunge wa Jimbo la Kalambo, Mhe. Edefonsi Joackim Kanoni , ameshiriki mazishi ya wananchi wawili waliofariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea katika Kijiji cha Kazila, Kata ya Mwazye, Wilaya ya Kalambo, huku akitoa pole na faraja kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki pamoja na wananchi wote walioguswa na msiba huo. Ajali hiyo ilitokea tarehe 05 Agosti 2026 , wakati gari aina ya Fuso lililokuwa limebeba watu waliokuwa wakielekea kwenye shughuli ya harusi kutoka Kijiji cha Msoma, Kata ya Mwazye, Wilaya ya Kalambo , lilipofika katika Kijiji cha Kazila kwa ajili ya shughuli ya kufunga ndoa. Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa, gari hilo lilikuwa limembeba bwana harusi, Hosea Gilbert Watua , pamoja na watu wengine waliokuwa wakisafiri naye kutoka Kijiji cha Msoma kuelekea Kijiji cha Kazila, ambako alikuwa akienda kufunga ndoa na bibi harusi, Mehili Sauli Visent , mkazi wa Kijiji cha Kazila, Kata ya Mwazye. AJALI YATOKEA KABLA YA KUFIKA KWENYE DARAJA Taarifa zinaeleza ...