Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, kwa kushirikiana na Atilis Investment Limited, inawataarifu Watanzania wenye sifa stahiki kuhusu nafasi 200 za ajira za mafundi katika sekta ya ujenzi, zilizotolewa na kampuni ya Shade Corporation Limited ya nchini Saudi Arabia.
KADA ZINAZOHITAJIKA
Nafasi hizo zinahusisha mafundi wa kada mbalimbali, wakiwemo:
- Mafundi Uashi
- Mafundi Useremala
- Wasuka Nondo
SIFA ZA MWOMBAJI
Mwombaji anatakiwa kuwa na:
- Elimu ya astashahada kutoka chuo cha ufundi kinachotambuliwa na Serikali;
- Uzoefu wa kazi wa miaka miwili (2) au zaidi katika sekta ya ufundi;
- Uwezo na uzoefu katika kada husika, ikiwemo Uashi, Useremala au Usuka Nondo;
- Umri kati ya miaka 21 hadi 40;
- Waombaji wa nafasi hizi wanatakiwa kuwa wanaume.
MASHARTI NA MAFANO YA AJIRA
Waombaji watakaofaulu mchakato wa ajira watapata fursa ya kufanya kazi nchini Saudi Arabia kwa masharti yaliyowekwa na mwajiri.
Miongoni mwa mafao na masharti ya ajira ni:
- Mshahara wa Riyal 1,100 za Saudi Arabia kwa mwezi;
- Posho ya chakula ya Riyal 275 kwa mwezi;
- Mwajiri kugharamia matibabu katika kipindi chote cha ajira;
- Mwajiri kugharamia usafiri kutoka eneo la makazi ya mfanyakazi hadi kituo cha kazi katika kipindi cha ajira;
- Mwajiri kugharamia tiketi ya ndege ya kwenda Saudi Arabia na kurudi baada ya mkataba kuisha;
- Mwajiri kugharamia malazi katika kipindi chote cha ajira.
Mkataba wa ajira utakuwa wa miezi sita (6) na unaweza kuhuishwa kwa makubaliano na masharti ya mwajiri.
JINSI YA KUTUMA MAOMBI
Waombaji wanatakiwa kutuma CV pamoja na nakala za vyeti vya taaluma kupitia barua pepe:
Baada ya kutuma maombi, mwombaji anatakiwa pia kujisajili kupitia mfumo wa ajira wa Serikali:
jobs.kazi.go.tz
Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 30 Agosti 2026.
TAREHE NA ENEO LA USAILI
Usaili utafanyika tarehe:
31 Agosti 2026 na 1 Septemba 2026
Eneo:
Itumbi Hotel – Ghorofa ya 5, Magomeni Mwembechai, Dar es Salaam.
MAWASILIANO
Kwa maelezo zaidi, waombaji wanaweza kuwasiliana kupitia:
Simu:
+255 711 707 500
+255 781 182 914
Tovuti:
jobs.kazi.go.tz
Tangazo hili limetolewa kwa ushirikiano na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, likiwa na lengo la kuwawezesha Watanzania wenye sifa kupata fursa za ajira katika sekta ya ujenzi nchini Saudi Arabia.
TAARIFA KWA WAKAZI WA WILAYA YA KALAMBO
Kwa waombaji kutoka Wilaya ya Kalambo wanaotuma maombi ya nafasi hizi, wanashauriwa kutoa taarifa kwa Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Kalambo ili Ofisi iwe na taarifa za waombaji kutoka Jimbo la Kalambo na iweze kusaidia katika ufuatiliaji wa mchakato pale inapohitajika.
Mawasiliano ya Ofisi ya Mbunge Jimbo la Kalambo
Simu: 0625850656
Barua pepe: [email protected]
Tovuti: www.mbungekalambo.com


💬 Toa Maoni Kuhusu Habari Hii
Umemaliza kusoma habari hii? Tupe maoni, mtazamo au swali lako hapa chini.
Comments
Post a Comment