📰 HABARI MPYA
Inapakia habari...

Disclaimer

KANUSHO (DISCLAIMER)

Tarehe ya Kuanza Kutumika: 26 Juni 2026

Taarifa zote zinazopatikana kwenye www.mbungekalambo.com zinachapishwa kwa nia njema na kwa madhumuni ya kutoa taarifa kwa wananchi.

Ingawa tunajitahidi kuhakikisha taarifa zote ni sahihi na zinasasishwa mara kwa mara, hatutoi dhamana kwamba taarifa zote zitakuwa:

  • Sahihi kwa asilimia 100
  • Kamili
  • Zinazoendana na wakati wote
  • Bila makosa

Mtumiaji anatumia taarifa zilizopo kwenye tovuti hii kwa hiari yake mwenyewe.

Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Kalambo haitawajibika kwa hasara yoyote itakayotokana na matumizi ya taarifa zilizopo kwenye tovuti hii.

Tovuti inaweza kuwa na viungo vya kuelekeza kwenye tovuti nyingine ambazo hatuzidhibiti.

Hatuhusiki na maudhui, sera wala huduma zinazotolewa na tovuti hizo.

Matangazo yanayoonekana kwenye tovuti yanatolewa na wahusika wengine.

Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Kalambo haiidhinishi wala kuwajibika kwa bidhaa au huduma zinazotangazwa.

Tunayo haki ya kubadilisha maudhui ya tovuti pamoja na Kanusho hili wakati wowote bila taarifa ya awali.

Kwa kutumia tovuti hii, unakubali Kanusho hili.


DISCLAIMER

(English Version)

The information published on www.mbungekalambo.com is provided in good faith for general informational purposes only.

While we strive to keep the information accurate and up to date, we make no warranties regarding its completeness, reliability or accuracy.

Any action you take based on information found on this website is strictly at your own risk.

The Office of the Member of Parliament for Kalambo Constituency shall not be liable for any loss or damage arising from the use of this website.

This website may contain links to external websites beyond our control.

We are not responsible for the content, privacy policies or practices of any third-party websites.

Advertisements displayed on this website are provided by third-party advertising partners. We do not endorse or guarantee the products or services advertised.

We reserve the right to modify this Disclaimer at any time without prior notice.

By using this website, you agree to this Disclaimer.

MATUKIO KWA NJIA YA PICHA

Inapakia picha...

HABARI MAARUFU

ZIARA YA MHE. KANONI KATIKA JIMBO LA KALAMBO IMEAIRISHWA; HIKI NDICHO KILICHOSABABISHA.

  Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Kalambo, Mhe. Edefonsi Joackim Kanoni , inapenda kuwataarifu wananchi wote wa Jimbo la Kalambo na umma kwa ujumla kuwa ziara iliyokuwa imepangwa kufanyika kuanzia tarehe 20 Julai 2026 hadi tarehe 10 Agosti 2026 imeahirishwa. Uamuzi huo umetokana na zuio la Serikali kuhusu kufanyika kwa mikutano ya hadhara katika kipindi hiki. Ofisi ya Mbunge inaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza na inaendelea kuwashukuru wananchi kwa ushirikiano na uelewa wao. Kwa taarifa zaidi na maendeleo ya shughuli za Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Kalambo, tembelea: www.mbungekalambo.com Imetolewa na: Musa Frackison Mzopola Katibu wa Mbunge, Jimbo la Kalambo

HATIMAYE! ORODHA RASMI YA WANUFAIKA WA MIKOPO YA WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI KWA WILAYA YA KALAMBO YATOLEWA – WANUFAIKA WOTE WATAKIWA KUHUDHURIA MAFUNZO MUHIMU

  TAARIFA KWA UMMA Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Kalambo, Mhe. Edefonsi Joackim Kanoni , inapenda kuwajulisha wananchi wote wa Wilaya ya Kalambo kuwa Wizara ya Mifugo na Uvuvi imekamilisha mapitio ya maombi ya mikopo yaliyowasilishwa na wananchi wa Wilaya ya Kalambo kupitia programu ya uwezeshaji wa wananchi kiuchumi. Kutokana na mchakato huo, Wizara imetoa rasmi orodha ya wanufaika waliokidhi vigezo na kufanikiwa kupata mikopo hiyo. Wanufaika kutoka Wilaya ya Kalambo ni kama ilivyoainishwa katika orodha rasmi ya Wizara, ambayo inajumuisha: Rahel John Mawela – Mradi wa Mbuzi Faustina Cladio Msumeno – Mradi wa Kuku wa Mayai William Isaya Moringe – Mradi wa Mbuzi Mashaka Medard Jastin – Mradi wa Mfumo wa Ubaridi Aibini Leonard John – Mradi wa Mbuzi Britney Shadi Pandisha – Mradi wa Kuku wa Nyama Sisilia Augustino Michael – Mradi wa Mbuzi Ofisi ya Mbunge inawapongeza wanufaika wote kwa kufanikiwa kupata fursa hiyo muhimu na inawatakia mafanikio katika utekelezaji wa ...

ZIARA YA MIKUTANO YA HADHARA YA MHE. EDEFONSI JOACKIM KANONI MBUNGE JIMBO LA KALAMBO YATANGAZWA

  Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Kalambo inapenda kuwataarifu wananchi wote wa Jimbo la Kalambo kuwa Mhe. Edefonsi Joackim Kanoni (Mb), Mbunge wa Jimbo la Kalambo, atafanya ziara ya mikutano ya hadhara katika kata na vijiji mbalimbali vya jimbo kuanzia tarehe 20 Julai, 2026 hadi tarehe 10 Agosti, 2026, kwa mujibu wa ratiba iliyoambatanishwa.    Ziara hii inalenga kuimarisha mawasiliano kati ya Mbunge na wananchi kwa kukutana nao ana kwa ana, kusikiliza maoni, kero na changamoto zinazowakabili, pamoja na kupokea mapendekezo yatakayosaidia kuboresha huduma za kijamii na kuharakisha maendeleo ya Jimbo la Kalambo. Aidha, Mhe. Mbunge atatoa mrejesho kuhusu utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kueleza mipango ya maendeleo inayotarajiwa kutekelezwa katika maeneo mbalimbali ya jimbo. Wananchi watapata fursa ya kuuliza maswali, kutoa maoni yao na kushiriki katika kujadili masuala muhimu yanayohusu maendeleo ya kata na vijiji vyao. Ushiriki wa wananchi katika mikutano hii ni msingi m...