📰 HABARI MPYA
Inapakia habari...

KANONI SUPER BONANZA KUANZA JULAI 6–7, 2026 KALAMBO

KANONI SUPER BONANZA KUANZA JULAI 6–7, 2026 KALAMBO

 

Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Kalambo inapenda kuwataarifu wananchi wote wa Jimbo la Kalambo na Watanzania kwa ujumla kuwa Mheshimiwa Edifonsi Joackim Kanoni, Mbunge wa Jimbo la Kalambo, ameandaa bonanza kubwa la michezo litakalojulikana kwa jina la KANONI SUPER BONANZA, litakalofanyika kuanzia tarehe 06 Julai, 2026 hadi tarehe 07 Julai, 2026.

Bonanza hilo limeandaliwa kwa lengo la kuendeleza na kuhamasisha michezo, kukuza vipaji vya vijana, kuimarisha afya za wananchi, pamoja na kuendeleza umoja, mshikamano na ushirikiano miongoni mwa wananchi wa Jimbo la Kalambo.

Timu zitakazoshiriki katika bonanza hilo ni:

  • Matai FC

  • Chapakazi FC

  • Motochini VS

  • Nyota Njema FC

Uzinduzi rasmi wa KANONI SUPER BONANZA utafanyika tarehe 06 Julai, 2026, uwanja wa Kateka kata ya Matai wilaya Kalambo ambapo Mheshimiwa Edifonsi Joackim Kanoni, Mbunge wa Jimbo la Kalambo, atakuwa Mgeni Rasmi.

Akizungumzia maandalizi ya bonanza hilo, Mheshimiwa Kanoni amesema kuwa michezo ni nyenzo muhimu ya kuimarisha afya, kuibua vipaji, kujenga urafiki na kuimarisha mshikamano wa wananchi. Ameeleza kuwa Ofisi yake itaendelea kuwekeza katika maendeleo ya michezo kama sehemu ya kuwatumikia wananchi na kuwajengea vijana mazingira bora ya kukuza vipaji vyao.

Aidha, Ofisi ya Mbunge inawakaribisha wananchi wote wa Jimbo la Kalambo kujitokeza kwa wingi kushuhudia na kushiriki katika bonanza hilo ili kuendelea kuimarisha umoja, upendo na mshikamano ambao ni msingi wa maendeleo ya Jimbo letu.

Kazi na Utu, Tunasonga Mbele.

Imetolewa na:

MUSA FRACKISON MZOPOPA
Katibu wa Mbunge Jimbo la Kalambo

Umemaliza kusoma habari hii? Tupe maoni, mtazamo au swali lako hapa chini.

Comments

MATUKIO KWA NJIA YA PICHA

Inapakia picha...

HABARI MAARUFU

FURSA ZA MIKOPO YA VIJANA SASA HADHARANI OMBA SASA UJIKWAMUE KIUCHUMI

  Katika kutekeleza ahadi ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya kutoa shilingi bilioni 200 kwa vijana ndani ya siku 100 baada ya kuingia madarakani, Wizara ya Mifugo na Uvuvi inautangazia umma kuanza kwa Awamu ya Pili ya utoaji wa mikopo yenye masharti nafuu kwa vijana. Malengo ya mikopo hiyo ni kuwawezesha vijana kupata mitaji ya kuanzisha na kuendeleza biashara ndogo, biashara za kati na kampuni changa ili kujijengea kipato katika Sekta za Mifugo na Uvuvi. Mikopo hiyo itatolewa kwa njia ya vifaa na pembejeo za uzalishaji, ikiwemo ufugaji wa samaki kwa vizimba, ufugaji wa kuku (chotara, mayai na nyama), mbuzi, kondoo na nguruwe, pamoja na boti za kuhudumia vizimba, boti za uvuvi, zana za uvuvi, mifumo ya ubari (cold chain) katika mazao ya uvuvi, mifumo ya kulazisha vifaranga vya samaki, mifumo na vifaa vya uchakataji wa mazao ya uvuvi ikijumuisha makausho ya dagaa na mwani (dryers). Vigezo na maelekezo kwa waombaji ni kama ifuatavyo: i. Baru...

NAFASI 200 ZA AJIRA ZA MAFUNDI ZATANGAZWA KWA KAZI NCHINI SAUDI ARABIA

  Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, kwa kushirikiana na Atilis Investment Limited , inawataarifu Watanzania wenye sifa stahiki kuhusu nafasi 200 za ajira za mafundi katika sekta ya ujenzi , zilizotolewa na kampuni ya Shade Corporation Limited ya nchini Saudi Arabia. KADA ZINAZOHITAJIKA Nafasi hizo zinahusisha mafundi wa kada mbalimbali, wakiwemo: Mafundi Uashi Mafundi Useremala Wasuka Nondo SIFA ZA MWOMBAJI Mwombaji anatakiwa kuwa na: Elimu ya astashahada kutoka chuo cha ufundi kinachotambuliwa na Serikali; Uzoefu wa kazi wa miaka miwili (2) au zaidi katika sekta ya ufundi; Uwezo na uzoefu katika kada husika, ikiwemo Uashi, Useremala au Usuka Nondo; Umri kati ya miaka 21 hadi 40 ; Waombaji wa nafasi hizi wanatakiwa kuwa wanaume . MASHARTI NA MAFANO YA AJIRA Waombaji watakaofaulu mchakato wa ajira watapata fursa ya kufanya kazi nchini Saudi Arabia kwa masharti yaliyowekwa na mwajiri. Miongoni mwa mafao na masharti ya ajira ni: Mshahara wa Riyal 1...

MHE. MBUNGE KANONI ASHIRIKI MAZISHI YA WAATHIRIKA WA AJALI KAZILA, ATOA WITO WA UPENDO, UMOJA NA MSHIKAMANO

  KALAMBO: Mbunge wa Jimbo la Kalambo, Mhe. Edefonsi Joackim Kanoni , ameshiriki mazishi ya wananchi wawili waliofariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea katika Kijiji cha Kazila, Kata ya Mwazye, Wilaya ya Kalambo, huku akitoa pole na faraja kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki pamoja na wananchi wote walioguswa na msiba huo. Ajali hiyo ilitokea tarehe 05 Agosti 2026 , wakati gari aina ya Fuso lililokuwa limebeba watu waliokuwa wakielekea kwenye shughuli ya harusi kutoka Kijiji cha Msoma, Kata ya Mwazye, Wilaya ya Kalambo , lilipofika katika Kijiji cha Kazila kwa ajili ya shughuli ya kufunga ndoa. Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa, gari hilo lilikuwa limembeba bwana harusi, Hosea Gilbert Watua , pamoja na watu wengine waliokuwa wakisafiri naye kutoka Kijiji cha Msoma kuelekea Kijiji cha Kazila, ambako alikuwa akienda kufunga ndoa na bibi harusi, Mehili Sauli Visent , mkazi wa Kijiji cha Kazila, Kata ya Mwazye. AJALI YATOKEA KABLA YA KUFIKA KWENYE DARAJA Taarifa zinaeleza ...