📰 HABARI MPYA
Inapakia habari...

KIKUNDI CHA TUINUANE MADIBILA KUNUFAIKA NA MKOPO WA SHILINGI MILIONI 100 KWA AJILI YA UNUNUZI WA TRAKTA

KIKUNDI CHA TUINUANE MADIBILA KUNUFAIKA NA MKOPO WA SHILINGI MILIONI 100 KWA AJILI YA UNUNUZI WA TRAKTA

KALAMBO: Kikundi cha Tuinuane kilichopo katika Kijiji cha Madibila, Jimbo la Kalambo, kimefanikiwa kunufaika na mkopo wa Shilingi Milioni 100 kwa ajili ya ununuzi wa trekta aina ya New Holland, kupitia mpango wa mikopo wa Serikali unaotekelezwa kupitia Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana.

Kikundi hicho ni miongoni mwa wanufaika wa mpango wa mikopo wenye thamani ya Shilingi Bilioni 200, unaotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Upatikanaji wa mkopo huo umewezekana kwa juhudi za Mbunge wa Jimbo la Kalambo, Mhe. Edefonsi Joackim Kanoni, ambaye amesaidia kufuatilia na kuwezesha upatikanaji wa fursa hiyo kupitia Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana.

Trekta aina ya New Holland, ambayo ni miongoni mwa matrekta bora na imara, inatarajiwa kuongeza tija katika shughuli za kilimo, kupunguza changamoto za upatikanaji wa huduma za kilimo na kuchochea maendeleo ya kiuchumi kwa wanakikundi pamoja na wananchi wa Kalambo kwa ujumla.

Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Kalambo imetoa shukrani za dhati kwa Serikali ya Awamu ya Sita, chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kujali, kuthamini na kuunga mkono juhudi za maendeleo ya wananchi wa Kalambo.

Aidha, Ofisi ya Mbunge imetoa shukrani maalum kwa Mhe. Joel Arthur Nanauka, Waziri wa Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, pamoja na Mawaziri na watendaji wote wa Serikali, kwa juhudi na ushirikiano wao katika kuhakikisha wananchi wanapata fursa za kiuchumi na mikopo yenye tija.

Pamoja na mafanikio hayo, Ofisi ya Mbunge inaendelea kuiomba Serikali kuendelea kutoa na kuongeza fursa za mikopo kwa wananchi wa Kalambo, hususan mikopo ya vizimba katika Ziwa Tanganyika pamoja na mikopo ya ufugaji, ili kuwawezesha wananchi wengi zaidi kushiriki katika shughuli za uzalishaji na kujikwamua kiuchumi.

Ofisi ya Mbunge inatoa wito kwa wananchi wote wa Kalambo kuendelea kudumisha upendo, umoja na mshikamano, kwa kuwa umoja na mshikamano wa wananchi ni msingi muhimu katika kuendeleza na kuijenga Kalambo yenye maendeleo endelevu.

Imetolewa na:
MUSA FRACKISON MZOPOLA
KATIBU WA MBUNGE
JIMBO LA KALAMBO


Umemaliza kusoma habari hii? Tupe maoni, mtazamo au swali lako hapa chini.

Comments

MATUKIO KWA NJIA YA PICHA

Inapakia picha...

HABARI MAARUFU

FURSA ZA MIKOPO YA VIJANA SASA HADHARANI OMBA SASA UJIKWAMUE KIUCHUMI

  Katika kutekeleza ahadi ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya kutoa shilingi bilioni 200 kwa vijana ndani ya siku 100 baada ya kuingia madarakani, Wizara ya Mifugo na Uvuvi inautangazia umma kuanza kwa Awamu ya Pili ya utoaji wa mikopo yenye masharti nafuu kwa vijana. Malengo ya mikopo hiyo ni kuwawezesha vijana kupata mitaji ya kuanzisha na kuendeleza biashara ndogo, biashara za kati na kampuni changa ili kujijengea kipato katika Sekta za Mifugo na Uvuvi. Mikopo hiyo itatolewa kwa njia ya vifaa na pembejeo za uzalishaji, ikiwemo ufugaji wa samaki kwa vizimba, ufugaji wa kuku (chotara, mayai na nyama), mbuzi, kondoo na nguruwe, pamoja na boti za kuhudumia vizimba, boti za uvuvi, zana za uvuvi, mifumo ya ubari (cold chain) katika mazao ya uvuvi, mifumo ya kulazisha vifaranga vya samaki, mifumo na vifaa vya uchakataji wa mazao ya uvuvi ikijumuisha makausho ya dagaa na mwani (dryers). Vigezo na maelekezo kwa waombaji ni kama ifuatavyo: i. Baru...

NAFASI 200 ZA AJIRA ZA MAFUNDI ZATANGAZWA KWA KAZI NCHINI SAUDI ARABIA

  Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, kwa kushirikiana na Atilis Investment Limited , inawataarifu Watanzania wenye sifa stahiki kuhusu nafasi 200 za ajira za mafundi katika sekta ya ujenzi , zilizotolewa na kampuni ya Shade Corporation Limited ya nchini Saudi Arabia. KADA ZINAZOHITAJIKA Nafasi hizo zinahusisha mafundi wa kada mbalimbali, wakiwemo: Mafundi Uashi Mafundi Useremala Wasuka Nondo SIFA ZA MWOMBAJI Mwombaji anatakiwa kuwa na: Elimu ya astashahada kutoka chuo cha ufundi kinachotambuliwa na Serikali; Uzoefu wa kazi wa miaka miwili (2) au zaidi katika sekta ya ufundi; Uwezo na uzoefu katika kada husika, ikiwemo Uashi, Useremala au Usuka Nondo; Umri kati ya miaka 21 hadi 40 ; Waombaji wa nafasi hizi wanatakiwa kuwa wanaume . MASHARTI NA MAFANO YA AJIRA Waombaji watakaofaulu mchakato wa ajira watapata fursa ya kufanya kazi nchini Saudi Arabia kwa masharti yaliyowekwa na mwajiri. Miongoni mwa mafao na masharti ya ajira ni: Mshahara wa Riyal 1...

MHE. MBUNGE KANONI ASHIRIKI MAZISHI YA WAATHIRIKA WA AJALI KAZILA, ATOA WITO WA UPENDO, UMOJA NA MSHIKAMANO

  KALAMBO: Mbunge wa Jimbo la Kalambo, Mhe. Edefonsi Joackim Kanoni , ameshiriki mazishi ya wananchi wawili waliofariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea katika Kijiji cha Kazila, Kata ya Mwazye, Wilaya ya Kalambo, huku akitoa pole na faraja kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki pamoja na wananchi wote walioguswa na msiba huo. Ajali hiyo ilitokea tarehe 05 Agosti 2026 , wakati gari aina ya Fuso lililokuwa limebeba watu waliokuwa wakielekea kwenye shughuli ya harusi kutoka Kijiji cha Msoma, Kata ya Mwazye, Wilaya ya Kalambo , lilipofika katika Kijiji cha Kazila kwa ajili ya shughuli ya kufunga ndoa. Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa, gari hilo lilikuwa limembeba bwana harusi, Hosea Gilbert Watua , pamoja na watu wengine waliokuwa wakisafiri naye kutoka Kijiji cha Msoma kuelekea Kijiji cha Kazila, ambako alikuwa akienda kufunga ndoa na bibi harusi, Mehili Sauli Visent , mkazi wa Kijiji cha Kazila, Kata ya Mwazye. AJALI YATOKEA KABLA YA KUFIKA KWENYE DARAJA Taarifa zinaeleza ...