📰 HABARI MPYA
Inapakia habari...

MBUNGE WA JIMBO LA KALAMBO ATEKELEZA AHADI YA KUENDELEZA MICHEZO KWA KUKABIDHI MIPIRA KWA VIJANA WA KIJIJI CHA ULUMI

 MBUNGE WA JIMBO LA KALAMBO ATEKELEZA AHADI YA KUENDELEZA MICHEZO KWA KUKABIDHI MIPIRA KWA VIJANA WA KIJIJI CHA ULUMI


Katika kuendelea kutekeleza kwa vitendo ahadi zake kwa wananchi wa Jimbo la Kalambo, Mbunge wa Jimbo la Kalambo, Mhe. Edifonsi Joackim Kanoni, kupitia Katibu wake Ndugu Musa Frackison Mzopola, amekabidhi mipira mitano (5) ya mpira wa miguu kwa viongozi wa timu za Ulumi A na Ulumi B.

Msaada huo umetolewa kufuatia ombi lililotolewa na vijana wa kijiji hicho wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika mwezi Aprili, ambapo walimweleza Mbunge changamoto ya ukosefu wa vifaa vya michezo. Utekelezaji huu unaonesha dhamira ya kweli ya Mhe. Kanoni ya kusikiliza wananchi na kutekeleza ahadi alizozitoa kwa wakati.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo kwa niaba ya Mbunge, Ndugu Musa Frackison Mzopola alisema kuwa Mhe. Kanoni anatambua mchango mkubwa wa michezo katika kujenga afya, kuimarisha umoja wa vijana, kukuza vipaji na kuondoa vitendo vinavyoweza kuhatarisha amani na maendeleo ya jamii.

Aidha, amewatangazia wananchi wa Kalambo kuwa, kama Mhe Mbunge alivyoahidi kuanzia mwezi Julai ofisi ya Mbunge imeanza utaratibu wa kutoa vifaa vya michezo kwa vikundi na timu mbalimbali zilizoomba msaada huo katika maeneo tofauti ya Jimbo la Kalambo. Alisisitiza kuwa waombaji wote watapatiwa huduma hiyo hatua kwa hatua, hivyo aliwaomba waendelee kuwa na subira wakati taratibu za ugawaji zikiendelea.

Vilevile, alieleza kuwa Mhe. Mbunge anatarajia kuanza tena ziara za mikutano ya hadhara katika vijiji mbalimbali vya Jimbo la Kalambo. Katika ziara hizo, ataendelea kusikiliza kero za wananchi, kufuatilia utekelezaji wa ahadi alizotoa na kukabidhi misaada mbalimbali katika maeneo yaliyoiomba.

Kwa upande wake, aliwahimiza vijana kutumia vipaji vyao kama njia ya kujiletea maendeleo na kujiongezea kipato, huku akiwataka kujiepusha na vitendo vya uhalifu, matumizi ya dawa za kulevya na mambo yote yanayoweza kuvuruga amani, utulivu na mshikamano wa Taifa letu.

Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Kalambo inaendelea kuwahimiza wananchi wote kushirikiana na Serikali katika kuleta maendeleo ya Jimbo letu. Ushirikiano, umoja, upendo na mshikamano ndiyo msingi wa kufanikisha miradi ya maendeleo na kujenga Kalambo yenye ustawi kwa kizazi cha sasa na kijacho.

Mhe. Edifonsi Joackim Kanoni anaendelea kuwathibitishia wananchi kuwa yuko bega kwa bega nao katika kutatua changamoto zao na kuhakikisha ahadi zote zinazotekelezeka zinafanyiwa kazi kwa vitendo kwa manufaa ya wananchi wote.

KAZI NA UTU TUNASONGAMBELE

Imetolewa na:
Musa Frackison Mzopola
Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Kalambo

Umemaliza kusoma habari hii? Tupe maoni, mtazamo au swali lako hapa chini.

Comments

MATUKIO KWA NJIA YA PICHA

Inapakia picha...

HABARI MAARUFU

FURSA ZA MIKOPO YA VIJANA SASA HADHARANI OMBA SASA UJIKWAMUE KIUCHUMI

  Katika kutekeleza ahadi ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya kutoa shilingi bilioni 200 kwa vijana ndani ya siku 100 baada ya kuingia madarakani, Wizara ya Mifugo na Uvuvi inautangazia umma kuanza kwa Awamu ya Pili ya utoaji wa mikopo yenye masharti nafuu kwa vijana. Malengo ya mikopo hiyo ni kuwawezesha vijana kupata mitaji ya kuanzisha na kuendeleza biashara ndogo, biashara za kati na kampuni changa ili kujijengea kipato katika Sekta za Mifugo na Uvuvi. Mikopo hiyo itatolewa kwa njia ya vifaa na pembejeo za uzalishaji, ikiwemo ufugaji wa samaki kwa vizimba, ufugaji wa kuku (chotara, mayai na nyama), mbuzi, kondoo na nguruwe, pamoja na boti za kuhudumia vizimba, boti za uvuvi, zana za uvuvi, mifumo ya ubari (cold chain) katika mazao ya uvuvi, mifumo ya kulazisha vifaranga vya samaki, mifumo na vifaa vya uchakataji wa mazao ya uvuvi ikijumuisha makausho ya dagaa na mwani (dryers). Vigezo na maelekezo kwa waombaji ni kama ifuatavyo: i. Baru...

NAFASI 200 ZA AJIRA ZA MAFUNDI ZATANGAZWA KWA KAZI NCHINI SAUDI ARABIA

  Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, kwa kushirikiana na Atilis Investment Limited , inawataarifu Watanzania wenye sifa stahiki kuhusu nafasi 200 za ajira za mafundi katika sekta ya ujenzi , zilizotolewa na kampuni ya Shade Corporation Limited ya nchini Saudi Arabia. KADA ZINAZOHITAJIKA Nafasi hizo zinahusisha mafundi wa kada mbalimbali, wakiwemo: Mafundi Uashi Mafundi Useremala Wasuka Nondo SIFA ZA MWOMBAJI Mwombaji anatakiwa kuwa na: Elimu ya astashahada kutoka chuo cha ufundi kinachotambuliwa na Serikali; Uzoefu wa kazi wa miaka miwili (2) au zaidi katika sekta ya ufundi; Uwezo na uzoefu katika kada husika, ikiwemo Uashi, Useremala au Usuka Nondo; Umri kati ya miaka 21 hadi 40 ; Waombaji wa nafasi hizi wanatakiwa kuwa wanaume . MASHARTI NA MAFANO YA AJIRA Waombaji watakaofaulu mchakato wa ajira watapata fursa ya kufanya kazi nchini Saudi Arabia kwa masharti yaliyowekwa na mwajiri. Miongoni mwa mafao na masharti ya ajira ni: Mshahara wa Riyal 1...

MHE. MBUNGE KANONI ASHIRIKI MAZISHI YA WAATHIRIKA WA AJALI KAZILA, ATOA WITO WA UPENDO, UMOJA NA MSHIKAMANO

  KALAMBO: Mbunge wa Jimbo la Kalambo, Mhe. Edefonsi Joackim Kanoni , ameshiriki mazishi ya wananchi wawili waliofariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea katika Kijiji cha Kazila, Kata ya Mwazye, Wilaya ya Kalambo, huku akitoa pole na faraja kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki pamoja na wananchi wote walioguswa na msiba huo. Ajali hiyo ilitokea tarehe 05 Agosti 2026 , wakati gari aina ya Fuso lililokuwa limebeba watu waliokuwa wakielekea kwenye shughuli ya harusi kutoka Kijiji cha Msoma, Kata ya Mwazye, Wilaya ya Kalambo , lilipofika katika Kijiji cha Kazila kwa ajili ya shughuli ya kufunga ndoa. Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa, gari hilo lilikuwa limembeba bwana harusi, Hosea Gilbert Watua , pamoja na watu wengine waliokuwa wakisafiri naye kutoka Kijiji cha Msoma kuelekea Kijiji cha Kazila, ambako alikuwa akienda kufunga ndoa na bibi harusi, Mehili Sauli Visent , mkazi wa Kijiji cha Kazila, Kata ya Mwazye. AJALI YATOKEA KABLA YA KUFIKA KWENYE DARAJA Taarifa zinaeleza ...