📰 HABARI MPYA
Inapakia habari...

MHE KANONI AIPONGEZA HALMASHAURI YA WILAYA YA KALAMBO YATOA MIKOPO YA ASILIMIA 10 YENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 50 KWA VIKUNDI

MHE KANONI AIPONGEZA HALMASHAURI YA WILAYA YA KALAMBO YATOA MIKOPO YA ASILIMIA 10 YENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 50 KWA VIKUNDI

 




Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Kalambo, Mhe. Edifonsi Joackim Kanoni, imepongeza Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo kwa kufanikisha utoaji wa mikopo ya asilimia 10 yenye thamani ya Shilingi milioni 50 kwa vikundi mbalimbali mwezi Mei 2026. Hatua hiyo inaonesha dhamira ya Serikali ya kuwawezesha wananchi kiuchumi, hususan vijana, wanawake na makundi maalum, kupitia fursa za mikopo kwa ajili ya kukuza shughuli za uzalishaji mali, kuongeza ajira na kuinua uchumi wa wananchi wa Wilaya ya Kalambo.

Vikundi vilivyonufaika na mikopo hiyo ni:

  1. Kikundi cha Wanawake Ilolesha – Kijiji cha Myunga, Kata ya Mkali – Shilingi 3,000,000.
  2. Kikundi cha Vijana Umoja ni Nguvu – Kijiji cha Mikonko, Kata ya Matai – Shilingi 10,000,000.
  3. Kikundi cha Walemavu – Kijiji cha Santamaria, Kata ya Lyowa – Shilingi 5,000,000.
  4. Kikundi cha Wanawake Ushindi – Kijiji cha Mao, Kata ya Mbuluma – Shilingi 8,000,000.
  5. Kikundi cha Ukuuwa Fashion – Kijiji cha Kasanga, Kata ya Kasanga – Shilingi 3,000,000.
  6. Kikundi cha Vijana Twaweza – Kijiji cha Mtula, Kata ya Mnamba – Shilingi 7,000,000.
  7. Kikundi cha Vijana Urafiki – Kijiji cha Kambo, Kata ya Kilesha – Shilingi 5,000,000.
  8. Agro-farm Group – Kijiji cha Kifone, Kata ya Kilesha – Shilingi 5,000,000.
  9. Kikundi cha Vijana cha Mito ya Baraka – Kijiji cha Kisala, Kata ya Samazi – Shilingi 4,000,000.

Jumla ya Shilingi milioni 50 zimetolewa kwa vikundi hivyo kwa lengo la kuongeza mitaji, kukuza shughuli za uzalishaji mali, kuongeza ajira na kuinua uchumi wa wananchi wa Wilaya ya Kalambo.

Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Kalambo inawahimiza vijana wengine kujitokeza kuunda vikundi vinavyokidhi vigezo ili waweze kunufaika na fursa za mikopo inayotolewa na Serikali. Vijana wanapaswa kuelekeza nguvu zao katika kufanya kazi kwa bidii, ubunifu na uzalendo, huku wakiepuka kujiingiza katika makundi yenye mienendo inayoweza kuvuruga amani, umoja na utulivu wa nchi yetu.

Aidha, Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Kalambo inatoa wito kwa wananchi wote wa Kalambo kuendelea kudumisha umoja, mshikamano na ushirikiano katika kuharakisha maendeleo ya wilaya. Maendeleo ya Kalambo yanategemea ushirikiano wa wananchi wote pamoja na matumizi sahihi ya fursa zinazotolewa na Serikali kwa manufaa ya jamii.

KAZI NA UTU TUNASONGA MBELE

Imetolewa na:

Musa Frackison Mzopola
Katibu wa Mbunge, Jimbo la Kalambo


Umemaliza kusoma habari hii? Tupe maoni, mtazamo au swali lako hapa chini.

Comments

MATUKIO KWA NJIA YA PICHA

Inapakia picha...

HABARI MAARUFU

FURSA ZA MIKOPO YA VIJANA SASA HADHARANI OMBA SASA UJIKWAMUE KIUCHUMI

  Katika kutekeleza ahadi ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya kutoa shilingi bilioni 200 kwa vijana ndani ya siku 100 baada ya kuingia madarakani, Wizara ya Mifugo na Uvuvi inautangazia umma kuanza kwa Awamu ya Pili ya utoaji wa mikopo yenye masharti nafuu kwa vijana. Malengo ya mikopo hiyo ni kuwawezesha vijana kupata mitaji ya kuanzisha na kuendeleza biashara ndogo, biashara za kati na kampuni changa ili kujijengea kipato katika Sekta za Mifugo na Uvuvi. Mikopo hiyo itatolewa kwa njia ya vifaa na pembejeo za uzalishaji, ikiwemo ufugaji wa samaki kwa vizimba, ufugaji wa kuku (chotara, mayai na nyama), mbuzi, kondoo na nguruwe, pamoja na boti za kuhudumia vizimba, boti za uvuvi, zana za uvuvi, mifumo ya ubari (cold chain) katika mazao ya uvuvi, mifumo ya kulazisha vifaranga vya samaki, mifumo na vifaa vya uchakataji wa mazao ya uvuvi ikijumuisha makausho ya dagaa na mwani (dryers). Vigezo na maelekezo kwa waombaji ni kama ifuatavyo: i. Baru...

NAFASI 200 ZA AJIRA ZA MAFUNDI ZATANGAZWA KWA KAZI NCHINI SAUDI ARABIA

  Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, kwa kushirikiana na Atilis Investment Limited , inawataarifu Watanzania wenye sifa stahiki kuhusu nafasi 200 za ajira za mafundi katika sekta ya ujenzi , zilizotolewa na kampuni ya Shade Corporation Limited ya nchini Saudi Arabia. KADA ZINAZOHITAJIKA Nafasi hizo zinahusisha mafundi wa kada mbalimbali, wakiwemo: Mafundi Uashi Mafundi Useremala Wasuka Nondo SIFA ZA MWOMBAJI Mwombaji anatakiwa kuwa na: Elimu ya astashahada kutoka chuo cha ufundi kinachotambuliwa na Serikali; Uzoefu wa kazi wa miaka miwili (2) au zaidi katika sekta ya ufundi; Uwezo na uzoefu katika kada husika, ikiwemo Uashi, Useremala au Usuka Nondo; Umri kati ya miaka 21 hadi 40 ; Waombaji wa nafasi hizi wanatakiwa kuwa wanaume . MASHARTI NA MAFANO YA AJIRA Waombaji watakaofaulu mchakato wa ajira watapata fursa ya kufanya kazi nchini Saudi Arabia kwa masharti yaliyowekwa na mwajiri. Miongoni mwa mafao na masharti ya ajira ni: Mshahara wa Riyal 1...

MHE. MBUNGE KANONI ASHIRIKI MAZISHI YA WAATHIRIKA WA AJALI KAZILA, ATOA WITO WA UPENDO, UMOJA NA MSHIKAMANO

  KALAMBO: Mbunge wa Jimbo la Kalambo, Mhe. Edefonsi Joackim Kanoni , ameshiriki mazishi ya wananchi wawili waliofariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea katika Kijiji cha Kazila, Kata ya Mwazye, Wilaya ya Kalambo, huku akitoa pole na faraja kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki pamoja na wananchi wote walioguswa na msiba huo. Ajali hiyo ilitokea tarehe 05 Agosti 2026 , wakati gari aina ya Fuso lililokuwa limebeba watu waliokuwa wakielekea kwenye shughuli ya harusi kutoka Kijiji cha Msoma, Kata ya Mwazye, Wilaya ya Kalambo , lilipofika katika Kijiji cha Kazila kwa ajili ya shughuli ya kufunga ndoa. Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa, gari hilo lilikuwa limembeba bwana harusi, Hosea Gilbert Watua , pamoja na watu wengine waliokuwa wakisafiri naye kutoka Kijiji cha Msoma kuelekea Kijiji cha Kazila, ambako alikuwa akienda kufunga ndoa na bibi harusi, Mehili Sauli Visent , mkazi wa Kijiji cha Kazila, Kata ya Mwazye. AJALI YATOKEA KABLA YA KUFIKA KWENYE DARAJA Taarifa zinaeleza ...