📰 HABARI MPYA
Inapakia habari...

SERIKALI YAMJIBU MHE. KANONI KWA VITENDO; YATOA FEDHA ZA UJENZI WA MIRADI YA ELIMU KALAMBO

SERIKALI YAMJIBU MHE. KANONI KWA VITENDO; YATOA FEDHA ZA UJENZI WA MIRADI YA ELIMU KALAMBO

Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Kalambo, Mhe. Edefonsi Joackim Kanoni, inapenda kutoa shukrani za dhati kwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na Mawaziri, viongozi na watendaji wote wa Serikali kwa kuendelea kusikiliza na kutekeleza kwa vitendo maombi yaliyowasilishwa kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wa Jimbo la Kalambo.

Ofisi ya Mbunge imepokea kwa furaha taarifa ya kutolewa kwa fedha za utekelezaji wa miradi mbalimbali ya elimu, ikiwa ni pamoja na ujenzi wa madarasa matano (5) na matundu kumi (10) ya vyoo katika Shule ya Msingi Msoma, Kata ya Mwazye, ujenzi wa madarasa matano (5) na matundu kumi (10) ya vyoo katika Shule ya Msingi Mzungwa, Kata ya Mambwenkoswe, pamoja na fedha za ujenzi wa Kituo cha Walimu katika Kijiji cha Kalembe, Kata ya Mambwenkoswe 

Hatua hii ni uthibitisho kuwa Serikali inaendelea kuwajali na kuwathamini wananchi wa Kalambo kwa kutekeleza miradi yenye lengo la kuboresha huduma za elimu na kuinua ustawi wa jamii.

Pamoja na mafanikio hayo, Ofisi ya Mbunge inaendelea kuiomba Serikali kuidhinisha fedha zaidi kwa ajili ya kukamilisha miradi mingine ya maendeleo ambayo imewasilishwa, ili wananchi wa Kalambo waendelee kunufaika na huduma bora katika sekta mbalimbali.

Aidha, Mhe. Kanoni anatoa wito kwa wananchi wote wa Jimbo la Kalambo kuendelea kudumisha umoja, upendo, mshikamano na ushirikiano, kwani maendeleo ya kweli yanapatikana pale wananchi wanaposhirikiana na kuunga mkono juhudi za Serikali katika kutekeleza miradi ya maendeleo.

Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Kalambo inaendelea kuwahakikishia wananchi kuwa itaendelea kusimamia na kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa ahadi na miradi yote ya maendeleo kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.

 

Imetolewa na


Musa Frackison Mzopola

Katibu wa Mbunge Jimbo la Kalambo

Umemaliza kusoma habari hii? Tupe maoni, mtazamo au swali lako hapa chini.

Comments

MATUKIO KWA NJIA YA PICHA

Inapakia picha...

HABARI MAARUFU

FURSA ZA MIKOPO YA VIJANA SASA HADHARANI OMBA SASA UJIKWAMUE KIUCHUMI

  Katika kutekeleza ahadi ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya kutoa shilingi bilioni 200 kwa vijana ndani ya siku 100 baada ya kuingia madarakani, Wizara ya Mifugo na Uvuvi inautangazia umma kuanza kwa Awamu ya Pili ya utoaji wa mikopo yenye masharti nafuu kwa vijana. Malengo ya mikopo hiyo ni kuwawezesha vijana kupata mitaji ya kuanzisha na kuendeleza biashara ndogo, biashara za kati na kampuni changa ili kujijengea kipato katika Sekta za Mifugo na Uvuvi. Mikopo hiyo itatolewa kwa njia ya vifaa na pembejeo za uzalishaji, ikiwemo ufugaji wa samaki kwa vizimba, ufugaji wa kuku (chotara, mayai na nyama), mbuzi, kondoo na nguruwe, pamoja na boti za kuhudumia vizimba, boti za uvuvi, zana za uvuvi, mifumo ya ubari (cold chain) katika mazao ya uvuvi, mifumo ya kulazisha vifaranga vya samaki, mifumo na vifaa vya uchakataji wa mazao ya uvuvi ikijumuisha makausho ya dagaa na mwani (dryers). Vigezo na maelekezo kwa waombaji ni kama ifuatavyo: i. Baru...

NAFASI 200 ZA AJIRA ZA MAFUNDI ZATANGAZWA KWA KAZI NCHINI SAUDI ARABIA

  Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, kwa kushirikiana na Atilis Investment Limited , inawataarifu Watanzania wenye sifa stahiki kuhusu nafasi 200 za ajira za mafundi katika sekta ya ujenzi , zilizotolewa na kampuni ya Shade Corporation Limited ya nchini Saudi Arabia. KADA ZINAZOHITAJIKA Nafasi hizo zinahusisha mafundi wa kada mbalimbali, wakiwemo: Mafundi Uashi Mafundi Useremala Wasuka Nondo SIFA ZA MWOMBAJI Mwombaji anatakiwa kuwa na: Elimu ya astashahada kutoka chuo cha ufundi kinachotambuliwa na Serikali; Uzoefu wa kazi wa miaka miwili (2) au zaidi katika sekta ya ufundi; Uwezo na uzoefu katika kada husika, ikiwemo Uashi, Useremala au Usuka Nondo; Umri kati ya miaka 21 hadi 40 ; Waombaji wa nafasi hizi wanatakiwa kuwa wanaume . MASHARTI NA MAFANO YA AJIRA Waombaji watakaofaulu mchakato wa ajira watapata fursa ya kufanya kazi nchini Saudi Arabia kwa masharti yaliyowekwa na mwajiri. Miongoni mwa mafao na masharti ya ajira ni: Mshahara wa Riyal 1...

MHE. MBUNGE KANONI ASHIRIKI MAZISHI YA WAATHIRIKA WA AJALI KAZILA, ATOA WITO WA UPENDO, UMOJA NA MSHIKAMANO

  KALAMBO: Mbunge wa Jimbo la Kalambo, Mhe. Edefonsi Joackim Kanoni , ameshiriki mazishi ya wananchi wawili waliofariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea katika Kijiji cha Kazila, Kata ya Mwazye, Wilaya ya Kalambo, huku akitoa pole na faraja kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki pamoja na wananchi wote walioguswa na msiba huo. Ajali hiyo ilitokea tarehe 05 Agosti 2026 , wakati gari aina ya Fuso lililokuwa limebeba watu waliokuwa wakielekea kwenye shughuli ya harusi kutoka Kijiji cha Msoma, Kata ya Mwazye, Wilaya ya Kalambo , lilipofika katika Kijiji cha Kazila kwa ajili ya shughuli ya kufunga ndoa. Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa, gari hilo lilikuwa limembeba bwana harusi, Hosea Gilbert Watua , pamoja na watu wengine waliokuwa wakisafiri naye kutoka Kijiji cha Msoma kuelekea Kijiji cha Kazila, ambako alikuwa akienda kufunga ndoa na bibi harusi, Mehili Sauli Visent , mkazi wa Kijiji cha Kazila, Kata ya Mwazye. AJALI YATOKEA KABLA YA KUFIKA KWENYE DARAJA Taarifa zinaeleza ...