Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Kalambo, Mhe. Edefonsi Joackim Kanoni, inapenda kuwataarifu wananchi wote wa Jimbo la Kalambo na umma kwa ujumla kuwa ziara iliyokuwa imepangwa kufanyika kuanzia tarehe 20 Julai 2026 hadi tarehe 10 Agosti 2026 imeahirishwa.
Uamuzi huo umetokana na zuio la Serikali kuhusu kufanyika kwa mikutano ya hadhara katika kipindi hiki.
Ofisi ya Mbunge inaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza na inaendelea kuwashukuru wananchi kwa ushirikiano na uelewa wao.
Kwa taarifa zaidi na maendeleo ya shughuli za Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Kalambo, tembelea: www.mbungekalambo.com
Imetolewa na:
Musa Frackison Mzopola
Katibu wa Mbunge, Jimbo la Kalambo

