📰 HABARI MPYA
Inapakia habari...

ZIARA YA MIKUTANO YA HADHARA YA MHE. EDEFONSI JOACKIM KANONI MBUNGE JIMBO LA KALAMBO YATANGAZWA

ZIARA YA MIKUTANO YA HADHARA YA MHE. EDEFONSI JOACKIM KANONI MBUNGE JIMBO LA KALAMBO YATANGAZWA

 

Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Kalambo inapenda kuwataarifu wananchi wote wa Jimbo la Kalambo kuwa Mhe. Edefonsi Joackim Kanoni (Mb), Mbunge wa Jimbo la Kalambo, atafanya ziara ya mikutano ya hadhara katika kata na vijiji mbalimbali vya jimbo kuanzia tarehe 20 Julai, 2026 hadi tarehe 10 Agosti, 2026, kwa mujibu wa ratiba iliyoambatanishwa.   

Ziara hii inalenga kuimarisha mawasiliano kati ya Mbunge na wananchi kwa kukutana nao ana kwa ana, kusikiliza maoni, kero na changamoto zinazowakabili, pamoja na kupokea mapendekezo yatakayosaidia kuboresha huduma za kijamii na kuharakisha maendeleo ya Jimbo la Kalambo. Aidha, Mhe. Mbunge atatoa mrejesho kuhusu utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kueleza mipango ya maendeleo inayotarajiwa kutekelezwa katika maeneo mbalimbali ya jimbo.

Wananchi watapata fursa ya kuuliza maswali, kutoa maoni yao na kushiriki katika kujadili masuala muhimu yanayohusu maendeleo ya kata na vijiji vyao. Ushiriki wa wananchi katika mikutano hii ni msingi muhimu wa uongozi shirikishi na maendeleo endelevu.

Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Kalambo inawaomba wananchi wote kujitokeza kwa wingi katika mikutano hiyo kulingana na ratiba ifuatayo ili waweze kumsikia Mbunge wao, kutoa maoni yao na kushiriki kikamilifu katika kujenga maendeleo ya Jimbo la Kalambo.



RATIBA YA MIKUTANO YA HADHARA

Tarehe: 20 Julai 2026 – 10 Agosti 2026

20/07/2026: Kata ya Samazi – Vijiji vya Kipanga, Katili na Samazi. 

21/07/2026: Kata ya Kasanga – Vijiji vya Kipwa na Kapele. 

22/07/2026: Kata ya Kasanga na Kisumba – Vijiji vya Kilewani na Kisumba. 

23/07/2026: Kata ya Mpomwe – Vijiji vya Nondo, Kapozwa na Mpomwe. 

24/07/2026: Kata ya Mkowe – Vijiji vya Limba, Mkowe A na Mkowe B. 

25/07/2026: Kata za Mkowe na Lyowa – Vijiji vya Katapulo, Mbuza na Santamaria. 

26/07/2026: Kata ya Katazi – Vijiji vya Kafukula, Katazi na Mvula. 

27/07/2026: Kata ya Mwazye – Vijiji vya Mpenje, Msoma na Kazila. 

28/07/2026: Kata ya Kilesha – Vijiji vya Itekesha, Kambo na Kifone. 

29/07/2026: Kata za Lyowa na Msanzi – Vijiji vya Singiwe, Msanzi Kati na Mbuluma. 

30/07/2026: Kata za Katete na Sopa – Vijiji vya Jengeni, Kasitu na Mtuntumbe. 

31/07/2026: Kata ya Mkali – Vijiji vya Kizombwe, Kalalasi na Myunga. 

01/08/2026: Kata ya Katete – Vijiji vya Kaluko, Ngoma na Katete. 

02/08/2026: Kata ya Sundu – Vijiji vya Kalaela, Kamawe na Zyangoma. 

03/08/2026: Kata ya Mwimbi – Vijiji vya Mozi, Selengoma na Msishindwe. 

04/08/2026: Kata ya Kanyezi – Vijiji vya Chalatila, Chisambo na Majengo. 

05/08/2026: Kata ya Matai/Nkonswe – Vijiji vya Tunyi, Mzungwa na Kasusu. 

06/08/2026: Kata ya Legezamwendo – Vijiji vya Mlenje, Mkombo na Legezamwendo. 

10/08/2026: Kata ya Ulumi – Vijiji vya Mnazi, Kale na Ulumi B. 

Imetolewa na:

Musa Frackison Mzopola

Katibu wa Mbunge

Jimbo la Kalambo

Umemaliza kusoma habari hii? Tupe maoni, mtazamo au swali lako hapa chini.

Comments

MATUKIO KWA NJIA YA PICHA

Inapakia picha...

HABARI MAARUFU

FURSA ZA MIKOPO YA VIJANA SASA HADHARANI OMBA SASA UJIKWAMUE KIUCHUMI

  Katika kutekeleza ahadi ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya kutoa shilingi bilioni 200 kwa vijana ndani ya siku 100 baada ya kuingia madarakani, Wizara ya Mifugo na Uvuvi inautangazia umma kuanza kwa Awamu ya Pili ya utoaji wa mikopo yenye masharti nafuu kwa vijana. Malengo ya mikopo hiyo ni kuwawezesha vijana kupata mitaji ya kuanzisha na kuendeleza biashara ndogo, biashara za kati na kampuni changa ili kujijengea kipato katika Sekta za Mifugo na Uvuvi. Mikopo hiyo itatolewa kwa njia ya vifaa na pembejeo za uzalishaji, ikiwemo ufugaji wa samaki kwa vizimba, ufugaji wa kuku (chotara, mayai na nyama), mbuzi, kondoo na nguruwe, pamoja na boti za kuhudumia vizimba, boti za uvuvi, zana za uvuvi, mifumo ya ubari (cold chain) katika mazao ya uvuvi, mifumo ya kulazisha vifaranga vya samaki, mifumo na vifaa vya uchakataji wa mazao ya uvuvi ikijumuisha makausho ya dagaa na mwani (dryers). Vigezo na maelekezo kwa waombaji ni kama ifuatavyo: i. Baru...

NAFASI 200 ZA AJIRA ZA MAFUNDI ZATANGAZWA KWA KAZI NCHINI SAUDI ARABIA

  Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, kwa kushirikiana na Atilis Investment Limited , inawataarifu Watanzania wenye sifa stahiki kuhusu nafasi 200 za ajira za mafundi katika sekta ya ujenzi , zilizotolewa na kampuni ya Shade Corporation Limited ya nchini Saudi Arabia. KADA ZINAZOHITAJIKA Nafasi hizo zinahusisha mafundi wa kada mbalimbali, wakiwemo: Mafundi Uashi Mafundi Useremala Wasuka Nondo SIFA ZA MWOMBAJI Mwombaji anatakiwa kuwa na: Elimu ya astashahada kutoka chuo cha ufundi kinachotambuliwa na Serikali; Uzoefu wa kazi wa miaka miwili (2) au zaidi katika sekta ya ufundi; Uwezo na uzoefu katika kada husika, ikiwemo Uashi, Useremala au Usuka Nondo; Umri kati ya miaka 21 hadi 40 ; Waombaji wa nafasi hizi wanatakiwa kuwa wanaume . MASHARTI NA MAFANO YA AJIRA Waombaji watakaofaulu mchakato wa ajira watapata fursa ya kufanya kazi nchini Saudi Arabia kwa masharti yaliyowekwa na mwajiri. Miongoni mwa mafao na masharti ya ajira ni: Mshahara wa Riyal 1...

MHE. MBUNGE KANONI ASHIRIKI MAZISHI YA WAATHIRIKA WA AJALI KAZILA, ATOA WITO WA UPENDO, UMOJA NA MSHIKAMANO

  KALAMBO: Mbunge wa Jimbo la Kalambo, Mhe. Edefonsi Joackim Kanoni , ameshiriki mazishi ya wananchi wawili waliofariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea katika Kijiji cha Kazila, Kata ya Mwazye, Wilaya ya Kalambo, huku akitoa pole na faraja kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki pamoja na wananchi wote walioguswa na msiba huo. Ajali hiyo ilitokea tarehe 05 Agosti 2026 , wakati gari aina ya Fuso lililokuwa limebeba watu waliokuwa wakielekea kwenye shughuli ya harusi kutoka Kijiji cha Msoma, Kata ya Mwazye, Wilaya ya Kalambo , lilipofika katika Kijiji cha Kazila kwa ajili ya shughuli ya kufunga ndoa. Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa, gari hilo lilikuwa limembeba bwana harusi, Hosea Gilbert Watua , pamoja na watu wengine waliokuwa wakisafiri naye kutoka Kijiji cha Msoma kuelekea Kijiji cha Kazila, ambako alikuwa akienda kufunga ndoa na bibi harusi, Mehili Sauli Visent , mkazi wa Kijiji cha Kazila, Kata ya Mwazye. AJALI YATOKEA KABLA YA KUFIKA KWENYE DARAJA Taarifa zinaeleza ...