📰 HABARI MPYA
Inapakia habari...

🚑 HATIMAYE! UKANDA WA MAMBWE WAPATA GARI LA WAGONJWA; RC CHARLES MAKONGORO NYERERE AFICHUA JINSI MBUNGE KANONI ALIVYOLIFUATILIA HADI KUPATIKANA

  🚑 HATIMAYE! UKANDA WA MAMBWE WAPATA GARI LA WAGONJWA; RC CHARLES MAKONGORO NYERERE AFICHUA JINSI MBUNGE KANONI ALIVYOLIFUATILIA HADI KUPATIKANA

Kalambo, Rukwa | Julai 29, 2026

Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Kalambo, Mhe. Edefonsi Joachim Kanoni, inapenda kuwajulisha wananchi wa Wilaya ya Kalambo kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imekabidhi rasmi gari jipya la wagonjwa kwa ajili ya kuhudumia wananchi wa Ukanda wa Mambwe.

Makabidhiano hayo yalifanyika tarehe 29 Julai, 2026 katika Kata ya Legezamwendo, yakiongozwa na Mhe. Charles Makongoro Nyerere, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa. Gari hilo linatarajiwa kuboresha huduma za dharura na kupunguza changamoto za usafirishaji wa wagonjwa katika Ukanda wa Mambwe.

Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano, Mhe. Charles Makongoro Nyerere aliwataka wananchi kulitunza gari hilo ili liweze kutoa huduma kwa muda mrefu. Aidha, aliwahimiza wananchi kumshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwajali wananchi wa Kalambo kupitia maboresho makubwa ya huduma za afya.

Kwa upande wa Wilaya ya Kalambo, Mkuu wa Mkoa aliwataka wananchi kumpongeza Mbunge wa Jimbo la Kalambo, Mhe. Edefonsi Joachim Kanoni, kwa juhudi zake za kuomba na kufuatilia kwa karibu upatikanaji wa gari hilo hadi kufanikisha kupatikana kwake.

Mhe. Charles Makongoro Nyerere alisema kuwa wakati Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Prof. Riziki Silas Shemdoe, alipofanya ziara mkoani Rukwa siku 14 zilizopita, alieleza kuwa Mbunge Kanoni ni mmoja wa wabunge wanaofuatilia kwa karibu mahitaji ya wananchi wao na hakuchoka kuwasilisha maombi serikalini, jambo lililochangia kupatikana kwa gari hilo.











Aidha, Mkuu wa Mkoa alisisitiza kuwa viongozi wanapaswa kuwa na utamaduni wa kufuatilia maendeleo ya wananchi badala ya kusubiri kila jambo lifike kwa utaratibu wa kawaida. Alibainisha kuwa kati ya magari 20 ya wagonjwa yaliyotolewa kwa Tanzania Bara, Mkoa wa Rukwa umefanikiwa kupata magari mawili kutokana na juhudi hizo.

Aliwahimiza pia wananchi kuendelea kushirikiana na Serikali kwa kujenga nyumba za watumishi wa afya ili kuwavutia na kuwawezesha kutoa huduma katika mazingira bora.

Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Kalambo, Mhe. Edefonsi Joachim Kanoni, alimshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuijali Kalambo kupitia uwekezaji mkubwa katika sekta ya afya. Vilevile alimshukuru Prof. Riziki Silas Shemdoe, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, pamoja na mawaziri, manaibu mawaziri na watendaji wote wa Serikali kwa ushirikiano walioutoa hadi kufanikisha upatikanaji wa gari hilo.

Mbunge Kanoni aliwahimiza wananchi kulitunza gari hilo ili kiendelee kuwahudumia kwa muda mrefu. Aidha, aliishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuendelea kuimarisha huduma za afya Wilayani Kalambo kupitia utoaji wa shilingi milioni 438 kwa ajili ya ukamilishaji wa Vituo vya Afya vya Legezamwendo, Mwazye na Samazi, pamoja na shilingi milioni 138 kwa ajili ya ukamilishaji wa Kituo cha Afya cha Kanyezi.

Mbunge huyo aliwaomba wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuwa imeendelea kuwajali na kuwathamini. Pia aliwasihi kuendeleza umoja, mshikamano na upendo ili kuharakisha maendeleo ya Wilaya ya Kalambo.

Kwa upande wao, wananchi wa Ukanda wa Mambwe walimshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mbunge Mhe. Edefonsi Joachim Kanoni, pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mhe. Charles Makongoro Nyerere, kwa kufanikisha upatikanaji wa gari hilo. Kama ishara ya shukrani na kuthamini juhudi hizo, wananchi walimkabidhi Mkuu wa Mkoa mbuzi.


KAZI NA UTU, TUNASONGA MBELE


Imetolewa na:


Musa Frackison Mzopola

Katibu wa Mbunge, Jimbo la Kalambo

Umemaliza kusoma habari hii? Tupe maoni, mtazamo au swali lako hapa chini.

Comments

MATUKIO KWA NJIA YA PICHA

Inapakia picha...

HABARI MAARUFU

FURSA ZA MIKOPO YA VIJANA SASA HADHARANI OMBA SASA UJIKWAMUE KIUCHUMI

  Katika kutekeleza ahadi ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya kutoa shilingi bilioni 200 kwa vijana ndani ya siku 100 baada ya kuingia madarakani, Wizara ya Mifugo na Uvuvi inautangazia umma kuanza kwa Awamu ya Pili ya utoaji wa mikopo yenye masharti nafuu kwa vijana. Malengo ya mikopo hiyo ni kuwawezesha vijana kupata mitaji ya kuanzisha na kuendeleza biashara ndogo, biashara za kati na kampuni changa ili kujijengea kipato katika Sekta za Mifugo na Uvuvi. Mikopo hiyo itatolewa kwa njia ya vifaa na pembejeo za uzalishaji, ikiwemo ufugaji wa samaki kwa vizimba, ufugaji wa kuku (chotara, mayai na nyama), mbuzi, kondoo na nguruwe, pamoja na boti za kuhudumia vizimba, boti za uvuvi, zana za uvuvi, mifumo ya ubari (cold chain) katika mazao ya uvuvi, mifumo ya kulazisha vifaranga vya samaki, mifumo na vifaa vya uchakataji wa mazao ya uvuvi ikijumuisha makausho ya dagaa na mwani (dryers). Vigezo na maelekezo kwa waombaji ni kama ifuatavyo: i. Baru...

NAFASI 200 ZA AJIRA ZA MAFUNDI ZATANGAZWA KWA KAZI NCHINI SAUDI ARABIA

  Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, kwa kushirikiana na Atilis Investment Limited , inawataarifu Watanzania wenye sifa stahiki kuhusu nafasi 200 za ajira za mafundi katika sekta ya ujenzi , zilizotolewa na kampuni ya Shade Corporation Limited ya nchini Saudi Arabia. KADA ZINAZOHITAJIKA Nafasi hizo zinahusisha mafundi wa kada mbalimbali, wakiwemo: Mafundi Uashi Mafundi Useremala Wasuka Nondo SIFA ZA MWOMBAJI Mwombaji anatakiwa kuwa na: Elimu ya astashahada kutoka chuo cha ufundi kinachotambuliwa na Serikali; Uzoefu wa kazi wa miaka miwili (2) au zaidi katika sekta ya ufundi; Uwezo na uzoefu katika kada husika, ikiwemo Uashi, Useremala au Usuka Nondo; Umri kati ya miaka 21 hadi 40 ; Waombaji wa nafasi hizi wanatakiwa kuwa wanaume . MASHARTI NA MAFANO YA AJIRA Waombaji watakaofaulu mchakato wa ajira watapata fursa ya kufanya kazi nchini Saudi Arabia kwa masharti yaliyowekwa na mwajiri. Miongoni mwa mafao na masharti ya ajira ni: Mshahara wa Riyal 1...

MHE. MBUNGE KANONI ASHIRIKI MAZISHI YA WAATHIRIKA WA AJALI KAZILA, ATOA WITO WA UPENDO, UMOJA NA MSHIKAMANO

  KALAMBO: Mbunge wa Jimbo la Kalambo, Mhe. Edefonsi Joackim Kanoni , ameshiriki mazishi ya wananchi wawili waliofariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea katika Kijiji cha Kazila, Kata ya Mwazye, Wilaya ya Kalambo, huku akitoa pole na faraja kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki pamoja na wananchi wote walioguswa na msiba huo. Ajali hiyo ilitokea tarehe 05 Agosti 2026 , wakati gari aina ya Fuso lililokuwa limebeba watu waliokuwa wakielekea kwenye shughuli ya harusi kutoka Kijiji cha Msoma, Kata ya Mwazye, Wilaya ya Kalambo , lilipofika katika Kijiji cha Kazila kwa ajili ya shughuli ya kufunga ndoa. Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa, gari hilo lilikuwa limembeba bwana harusi, Hosea Gilbert Watua , pamoja na watu wengine waliokuwa wakisafiri naye kutoka Kijiji cha Msoma kuelekea Kijiji cha Kazila, ambako alikuwa akienda kufunga ndoa na bibi harusi, Mehili Sauli Visent , mkazi wa Kijiji cha Kazila, Kata ya Mwazye. AJALI YATOKEA KABLA YA KUFIKA KWENYE DARAJA Taarifa zinaeleza ...