📰 HABARI MPYA
Inapakia habari...

MAMBO MAKUBWA YA ELIMU YALIYOFANYWA NA MHE. KANONI KALAMBO

MAMBO MAKUBWA YA ELIMU YALIYOFANYWA NA MHE. KANONI KALAMBO

 

KALAMBO: Katika kipindi cha uongozi wake, Mhe. Edefonce Joackim Kanoni, Mbunge wa Jimbo la Kalambo, ameendelea kuweka msukumo katika kuboresha sekta ya elimu kwa kuwasilisha changamoto za wananchi Serikalini na kufuatilia upatikanaji wa fedha kwa ajili ya miundombinu ya shule.

Miongoni mwa mambo makubwa yaliyofanyika ni ufuatiliaji wa umaliziaji wa magofu 143 ya vyumba vya madarasa, hatua inayolenga kuongeza nafasi za kujifunzia na kuboresha mazingira ya elimu katika maeneo mbalimbali ya Jimbo la Kalambo.

Kupitia Mfuko wa Jimbo, kiasi cha shilingi milioni 173 kilipatikana na kutumika katika miradi mbalimbali ya maendeleo, ambapo sehemu ya fedha hizo ilitumika katika umaliziaji wa vyumba 20 vya madarasa.

Aidha, Serikali imeingiza shilingi milioni 580 kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Sekondari Kanyezi, ikiwa ni hatua muhimu katika kuongeza miundombinu ya elimu na kuwasaidia wanafunzi kupata huduma ya elimu katika mazingira bora.

Mhe. Kanoni pia amewasilisha na kufuatilia ombi la ujenzi wa shule tatu za sekondari katika kata ya Kilesha Sundu na Lyowa ambazo bado hazina shule za sekondari, akisisitiza umuhimu wa kuhakikisha wanafunzi wanapata fursa ya kuendelea na elimu ya sekondari bila kulazimika kusafiri umbali mrefu.

Juhudi hizo zinaelezwa kuwa sehemu ya utekelezaji wa wajibu wa Mbunge wa kuwakilisha wananchi, kuwasilisha changamoto zao na kufuatilia hatua za Serikali katika kutatua changamoto za sekta ya elimu.

Kwa ujumla, hatua hizo zinaonyesha msukumo unaowekwa katika kuongeza miundombinu ya elimu, kupunguza changamoto ya vyumba vya madarasa na kuongeza upatikanaji wa shule za sekondari katika Jimbo la Kalambo.

ELIMU BORA, MSINGI WA MAENDELEO YA KALAMBO.


Imetolewa na:

Musa Frackison Mzopola

Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Kalambo

Umemaliza kusoma habari hii? Tupe maoni, mtazamo au swali lako hapa chini.

Comments

MATUKIO KWA NJIA YA PICHA

Inapakia picha...

HABARI MAARUFU

TANGAZO LA MIKOPO KWA VIJANA AWAMU YA PILI

  Katika kutekeleza ahadi ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya kutoa shilingi bilioni 200 kwa vijana ndani ya siku 100 baada ya kuingia madarakani, Wizara ya Mifugo na Uvuvi inautangazia umma kuanza kwa Awamu ya Pili ya utoaji wa mikopo yenye masharti nafuu kwa vijana. Malengo ya mikopo hiyo ni kuwawezesha vijana kupata mitaji ya kuanzisha na kuendeleza biashara ndogo, biashara za kati na kampuni changa ili kujijengea kipato katika Sekta za Mifugo na Uvuvi. Mikopo hiyo itatolewa kwa njia ya vifaa na pembejeo za uzalishaji, ikiwemo ufugaji wa samaki kwa vizimba, ufugaji wa kuku (chotara, mayai na nyama), mbuzi, kondoo na nguruwe, pamoja na boti za kuhudumia vizimba, boti za uvuvi, zana za uvuvi, mifumo ya ubari (cold chain) katika mazao ya uvuvi, mifumo ya kulazisha vifaranga vya samaki, mifumo na vifaa vya uchakataji wa mazao ya uvuvi ikijumuisha makausho ya dagaa na mwani (dryers). Vigezo na maelekezo kwa waombaji ni kama ifuatavyo: i. Baru...

MHE. MBUNGE KANONI ASHIRIKI MAZISHI YA WAATHIRIKA WA AJALI KAZILA, ATOA WITO WA UPENDO, UMOJA NA MSHIKAMANO

  KALAMBO: Mbunge wa Jimbo la Kalambo, Mhe. Edefonsi Joackim Kanoni , ameshiriki mazishi ya wananchi wawili waliofariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea katika Kijiji cha Kazila, Kata ya Mwazye, Wilaya ya Kalambo, huku akitoa pole na faraja kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki pamoja na wananchi wote walioguswa na msiba huo. Ajali hiyo ilitokea tarehe 05 Agosti 2026 , wakati gari aina ya Fuso lililokuwa limebeba watu waliokuwa wakielekea kwenye shughuli ya harusi kutoka Kijiji cha Msoma, Kata ya Mwazye, Wilaya ya Kalambo , lilipofika katika Kijiji cha Kazila kwa ajili ya shughuli ya kufunga ndoa. Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa, gari hilo lilikuwa limembeba bwana harusi, Hosea Gilbert Watua , pamoja na watu wengine waliokuwa wakisafiri naye kutoka Kijiji cha Msoma kuelekea Kijiji cha Kazila, ambako alikuwa akienda kufunga ndoa na bibi harusi, Mehili Sauli Visent , mkazi wa Kijiji cha Kazila, Kata ya Mwazye. AJALI YATOKEA KABLA YA KUFIKA KWENYE DARAJA Taarifa zinaeleza ...