📰 HABARI MPYA
Inapakia habari...

MHE. KANONI ATOA SALAMU ZA MAULIDI, AWASIHI WANAKALAMBO NA WATANZANIA KUDUMISHA AMANI

 MHE. KANONI ATOA SALAMU ZA MAULIDI, AWASIHI WANAKALAMBO NA WATANZANIA KUDUMISHA AMANI

 

Mhe. Edefonsi Joackim Kanoni, Mbunge wa Jimbo la Kalambo, amewatakia Wanakalambo na Watanzania wote, hususan Waislamu, Maulidi njema yenye furaha, upendo, mshikamano na amani.

Katika salamu zake za Maulidi, Mhe. Kanoni amesema sikukuu kama hii ni wakati muhimu wa kutafakari na kujikumbusha kumrudia Muumba wetu, kuishi kwa kufuata mafundisho mema, kutenda mema, kusaidiana na kuwa na upendo na huruma kwa wengine.

Amesema Maulidi inapaswa kuwa zaidi ya sherehe, bali iwe fursa ya kujenga jamii yenye maadili mema, upendo, umoja, mshikamano na amani, kwa kuwa mambo hayo ndiyo msingi wa maendeleo ya familia, jamii na taifa kwa ujumla.

Mhe. Kanoni amesisitiza umuhimu wa amani ya Tanzania, akieleza kuwa amani ni tunu kubwa ambayo kila Mtanzania anapaswa kuilinda na kuithamini.

Amesema iwapo amani itapotea, shughuli nyingi za kijamii, kiuchumi na hata za ibada zinaweza kusimama, jambo ambalo linaweza kuathiri uchumi na maendeleo ya nchi.

Katika maadhimisho haya ya Maulidi, Mhe. Kanoni amewaomba Watanzania kuwaombea viongozi wa nchi, ili waendelee kuiongoza Tanzania kwa hekima, upendo, mshikamano na kulinda amani ya taifa.

Ametoa wito kwa wananchi kuwaombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na Mawaziri, Naibu Mawaziri, Wabunge na viongozi wengine wa Serikali, ili Mungu awape hekima, afya na uwezo wa kulitumikia taifa kwa uadilifu na kuhakikisha amani na mshikamano vinaendelea kudumu.

Aidha, amewaomba Watanzania kuwaombea Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na watendaji wote wa Serikali, ili katika majukumu yao waweze kulitumikia taifa kwa weledi, uadilifu na kwa kuzingatia maslahi ya Watanzania.

Mhe. Kanoni amewataka Wanakalambo na Watanzania wote kutumia siku hii ya Maulidi kuimarisha udugu, kuvumiliana, kusaidiana na kuendeleza utamaduni wa kuishi pamoja kwa amani bila kujali tofauti za dini, itikadi au makundi.

Amesema Tanzania ni yetu sote, hivyo kila mmoja ana wajibu wa kuilinda amani, umoja na mshikamano ambao taifa limejenga kwa miaka mingi.

“Amani ndiyo tunu yetu. Tuilinde, tuiombee na tuiendeleze kwa vitendo, kwa sababu bila amani hakuna maendeleo endelevu.”

Mhe. Edefonsi Joackim Kanoni amewatakia Wanakalambo, Watanzania wote na Waislamu kote nchini Maulidi yenye baraka, akiwataka kutumia siku hiyo kutenda mema, kueneza upendo na kuendelea kumuomba Mwenyezi Mungu ailinde Tanzania na watu wake.

Maulidi Njema!

Amani, Upendo na Mshikamano kwa Taifa Letu.


Imetolewa na:

Musa Frackison Mzopola

Katibu wa Mbunge Jimbo la Kalambo

Umemaliza kusoma habari hii? Tupe maoni, mtazamo au swali lako hapa chini.

Comments

MATUKIO KWA NJIA YA PICHA

Inapakia picha...

HABARI MAARUFU

TANGAZO LA MIKOPO KWA VIJANA AWAMU YA PILI

  Katika kutekeleza ahadi ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya kutoa shilingi bilioni 200 kwa vijana ndani ya siku 100 baada ya kuingia madarakani, Wizara ya Mifugo na Uvuvi inautangazia umma kuanza kwa Awamu ya Pili ya utoaji wa mikopo yenye masharti nafuu kwa vijana. Malengo ya mikopo hiyo ni kuwawezesha vijana kupata mitaji ya kuanzisha na kuendeleza biashara ndogo, biashara za kati na kampuni changa ili kujijengea kipato katika Sekta za Mifugo na Uvuvi. Mikopo hiyo itatolewa kwa njia ya vifaa na pembejeo za uzalishaji, ikiwemo ufugaji wa samaki kwa vizimba, ufugaji wa kuku (chotara, mayai na nyama), mbuzi, kondoo na nguruwe, pamoja na boti za kuhudumia vizimba, boti za uvuvi, zana za uvuvi, mifumo ya ubari (cold chain) katika mazao ya uvuvi, mifumo ya kulazisha vifaranga vya samaki, mifumo na vifaa vya uchakataji wa mazao ya uvuvi ikijumuisha makausho ya dagaa na mwani (dryers). Vigezo na maelekezo kwa waombaji ni kama ifuatavyo: i. Baru...

MHE. MBUNGE KANONI ASHIRIKI MAZISHI YA WAATHIRIKA WA AJALI KAZILA, ATOA WITO WA UPENDO, UMOJA NA MSHIKAMANO

  KALAMBO: Mbunge wa Jimbo la Kalambo, Mhe. Edefonsi Joackim Kanoni , ameshiriki mazishi ya wananchi wawili waliofariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea katika Kijiji cha Kazila, Kata ya Mwazye, Wilaya ya Kalambo, huku akitoa pole na faraja kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki pamoja na wananchi wote walioguswa na msiba huo. Ajali hiyo ilitokea tarehe 05 Agosti 2026 , wakati gari aina ya Fuso lililokuwa limebeba watu waliokuwa wakielekea kwenye shughuli ya harusi kutoka Kijiji cha Msoma, Kata ya Mwazye, Wilaya ya Kalambo , lilipofika katika Kijiji cha Kazila kwa ajili ya shughuli ya kufunga ndoa. Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa, gari hilo lilikuwa limembeba bwana harusi, Hosea Gilbert Watua , pamoja na watu wengine waliokuwa wakisafiri naye kutoka Kijiji cha Msoma kuelekea Kijiji cha Kazila, ambako alikuwa akienda kufunga ndoa na bibi harusi, Mehili Sauli Visent , mkazi wa Kijiji cha Kazila, Kata ya Mwazye. AJALI YATOKEA KABLA YA KUFIKA KWENYE DARAJA Taarifa zinaeleza ...