📰 HABARI MPYA
Inapakia habari...

OFISI YA MBUNGE JIMBO LA KALAMBO YATOA POLE KWA KIFO CHA KIJANA BARACKA LEONARD MSILI

 OFISI YA MBUNGE JIMBO LA KALAMBO YATOA POLE KWA KIFO CHA KIJANA BARACKA LEONARD MSILI

 

Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Kalambo, Mhe. Edefonsi Joackim Kanoni, imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha kijana Baracka Leonard Msili, mkazi wa Santamaria, Wilaya ya Kalambo, Mkoa wa Rukwa, kilichotokea katika eneo hilo.

Katika kipindi hiki kigumu cha majonzi, Mhe. Edefonsi Joackim Kanoni anatoa pole za dhati kwa ndugu, jamaa, marafiki na wote walioguswa na msiba huu mkubwa.

Tunatambua kuwa kumpoteza kijana katika umri mdogo ni pigo kubwa kwa familia, ndugu na jamii kwa ujumla. Tunawaombea Mwenyezi Mungu awape nguvu, faraja na uvumilivu katika kipindi hiki cha majonzi, na ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.

Kifo kinatukumbusha kuwa maisha ya mwanadamu ni mafupi na hakuna anayejua siku wala saa yake. Hivyo, kila mmoja wetu anapaswa kuishi kwa kufanya mema, kujenga mahusiano mazuri na jamii, kusaidia wengine na kuweka alama njema katika maisha yake ili atakapoondoka duniani akumbukwe kwa mazuri aliyoyafanya.

Aidha, Ofisi ya Mbunge inatoa rai kwa madereva wote wa pikipiki na magari kuzingatia sheria na kanuni za usalama barabarani, kuwa makini wakati wote wanapokuwa barabarani na kuepuka vitendo vinavyoweza kusababisha ajali na kupoteza maisha.

Pia tunatoa wito kwa maafisa usalama barabarani kuendelea kusimamia sheria kwa ufanisi na kutoa elimu kwa watumiaji wa barabara, hususan vijana wanaotumia pikipiki, ili kusaidia kupunguza ajali na kulinda maisha ya wananchi.

Maisha ya kila mmoja yana thamani kubwa, hivyo ni jukumu letu sote kuhakikisha tunalinda maisha kwa kuchukua tahadhari na kuzingatia usalama katika kila hatua.

Imetolewa na:

Musa Frackison Mzopola
Katibu wa Mbunge Jimbo la Kalambo


Umemaliza kusoma habari hii? Tupe maoni, mtazamo au swali lako hapa chini.

Comments

MATUKIO KWA NJIA YA PICHA

Inapakia picha...

HABARI MAARUFU

TANGAZO LA MIKOPO KWA VIJANA AWAMU YA PILI

  Katika kutekeleza ahadi ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya kutoa shilingi bilioni 200 kwa vijana ndani ya siku 100 baada ya kuingia madarakani, Wizara ya Mifugo na Uvuvi inautangazia umma kuanza kwa Awamu ya Pili ya utoaji wa mikopo yenye masharti nafuu kwa vijana. Malengo ya mikopo hiyo ni kuwawezesha vijana kupata mitaji ya kuanzisha na kuendeleza biashara ndogo, biashara za kati na kampuni changa ili kujijengea kipato katika Sekta za Mifugo na Uvuvi. Mikopo hiyo itatolewa kwa njia ya vifaa na pembejeo za uzalishaji, ikiwemo ufugaji wa samaki kwa vizimba, ufugaji wa kuku (chotara, mayai na nyama), mbuzi, kondoo na nguruwe, pamoja na boti za kuhudumia vizimba, boti za uvuvi, zana za uvuvi, mifumo ya ubari (cold chain) katika mazao ya uvuvi, mifumo ya kulazisha vifaranga vya samaki, mifumo na vifaa vya uchakataji wa mazao ya uvuvi ikijumuisha makausho ya dagaa na mwani (dryers). Vigezo na maelekezo kwa waombaji ni kama ifuatavyo: i. Baru...

MHE. MBUNGE KANONI ASHIRIKI MAZISHI YA WAATHIRIKA WA AJALI KAZILA, ATOA WITO WA UPENDO, UMOJA NA MSHIKAMANO

  KALAMBO: Mbunge wa Jimbo la Kalambo, Mhe. Edefonsi Joackim Kanoni , ameshiriki mazishi ya wananchi wawili waliofariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea katika Kijiji cha Kazila, Kata ya Mwazye, Wilaya ya Kalambo, huku akitoa pole na faraja kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki pamoja na wananchi wote walioguswa na msiba huo. Ajali hiyo ilitokea tarehe 05 Agosti 2026 , wakati gari aina ya Fuso lililokuwa limebeba watu waliokuwa wakielekea kwenye shughuli ya harusi kutoka Kijiji cha Msoma, Kata ya Mwazye, Wilaya ya Kalambo , lilipofika katika Kijiji cha Kazila kwa ajili ya shughuli ya kufunga ndoa. Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa, gari hilo lilikuwa limembeba bwana harusi, Hosea Gilbert Watua , pamoja na watu wengine waliokuwa wakisafiri naye kutoka Kijiji cha Msoma kuelekea Kijiji cha Kazila, ambako alikuwa akienda kufunga ndoa na bibi harusi, Mehili Sauli Visent , mkazi wa Kijiji cha Kazila, Kata ya Mwazye. AJALI YATOKEA KABLA YA KUFIKA KWENYE DARAJA Taarifa zinaeleza ...