📰 HABARI MPYA
Inapakia habari...

SERIKALI YA AWAMU YA SITA YAENDELEA KUIMARISHA HUDUMA ZA AFYA KALAMBO KWA KUTENGA ZAIDI YA SHILINGI BILIONI 1.2

SERIKALI YA AWAMU YA SITA YAENDELEA KUIMARISHA HUDUMA ZA AFYA KALAMBO KWA KUTENGA ZAIDI YA SHILINGI BILIONI 1.2

 

Ofisi ya Mbunge Jimbo la Kalambo inapenda kuwataarifu wananchi wote wa Jimbo la Kalambo kuwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuonesha dhamira ya dhati ya kuboresha huduma za afya kwa kutenga zaidi ya shilingi bilioni 1.2 kwa ajili ya ujenzi na ukamilishaji wa vituo vya afya na zahanati mbalimbali ndani ya Jimbo la Kalambo.

Akizungumza wakati wa kukabidhi gari la wagonjwa (Ambulance) katika Kata ya Legezamwendo, Mbunge wa Jimbo la Kalambo, Mhe. Edefonsi Joackim Kanoni, amesema kuwa uwekezaji huo unaonesha wazi jinsi Serikali inavyoweka kipaumbele katika kuimarisha sekta ya afya kwa kusogeza huduma karibu na wananchi ili kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma bora, salama na kwa wakati. Amesema dhamira ya Serikali ni kuendelea kuboresha afya za wananchi, kupunguza vifo vinavyoweza kuzuilika, kuimarisha huduma za afya ya mama na mtoto, pamoja na kuongeza ustawi wa jamii kupitia huduma bora za matibabu.

Mhe. Kanoni amesema kuwa katika utekelezaji wa mpango huo, Serikali imetenga shilingi milioni 650 kupitia Serikali Kuu kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya Ulumi, shilingi milioni 300 kwa ajili ya umaliziaji wa Vituo vya Afya Mwazye na Legezamwendo, shilingi milioni 60 kutoka mapato ya Halmashauri kwa ajili ya umaliziaji wa Kituo cha Afya Samazi, shilingi milioni 138 kwa ajili ya umaliziaji wa Kituo cha Afya Kanyezi, pamoja na shilingi milioni 106 kwa ajili ya umaliziaji wa Zahanati ya Kijiji cha Tunyi, Kata ya Mambwenkoswe.

Amesema kukamilika kwa miradi hiyo kutapunguza adha ya wananchi kusafiri umbali mrefu kutafuta huduma za matibabu, kuboresha huduma za afya ya mama na mtoto, kuongeza uwezo wa kuhudumia wagonjwa wa dharura, kuimarisha mazingira ya kazi kwa watumishi wa afya na kuongeza upatikanaji wa huduma bora za afya kwa wananchi wote. Aidha, amesema uwekezaji huo utachochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa kuwa wananchi wenye afya njema hushiriki kikamilifu katika shughuli za uzalishaji na maendeleo ya Taifa.

Mbunge huyo ameishukuru kwa dhati Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuendelea kupeleka fedha za maendeleo katika Jimbo la Kalambo. Pia ametoa shukrani kwa Mawaziri, Manaibu Mawaziri, viongozi wa Mkoa wa Rukwa, Wilaya ya Kalambo pamoja na watendaji wote wa Serikali kwa ushirikiano mkubwa wanaouonesha katika kuhakikisha miradi ya maendeleo inatekelezwa na kuwanufaisha wananchi.

Aidha, Mhe. Kanoni amewaomba wananchi wa Jimbo la Kalambo kuendelea kusimamia kwa karibu utekelezaji wa miradi hiyo ili fedha zilizotengwa zitumike kwa uadilifu, uwazi na ufanisi. Amesisitiza kuwa fedha hizo ni mali ya wananchi zinazotokana na kodi zao, hivyo kila mwananchi ana wajibu wa kuzilinda na kuhakikisha miradi inakamilika kwa viwango vinavyokusudiwa.

Katika hitimisho la hotuba yake, Mhe. Kanoni ametoa wito kwa wananchi kuendelea kudumisha upendo, amani, umoja na mshikamano, akieleza kuwa misingi hiyo ndiyo nguzo muhimu ya maendeleo endelevu. Amesema kwa kuendelea kushirikiana na kuiunga mkono Serikali katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo, Jimbo la Kalambo litaendelea kupiga hatua kubwa za maendeleo.

KAZI NA UTU, TUNASONGA MBELE.

Imetolewa na:
Musa Frackison Mzopola
Katibu wa Mbunge Jimbo la Kalambo

Umemaliza kusoma habari hii? Tupe maoni, mtazamo au swali lako hapa chini.

Comments

MATUKIO KWA NJIA YA PICHA

Inapakia picha...

HABARI MAARUFU

FURSA ZA MIKOPO YA VIJANA SASA HADHARANI OMBA SASA UJIKWAMUE KIUCHUMI

  Katika kutekeleza ahadi ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya kutoa shilingi bilioni 200 kwa vijana ndani ya siku 100 baada ya kuingia madarakani, Wizara ya Mifugo na Uvuvi inautangazia umma kuanza kwa Awamu ya Pili ya utoaji wa mikopo yenye masharti nafuu kwa vijana. Malengo ya mikopo hiyo ni kuwawezesha vijana kupata mitaji ya kuanzisha na kuendeleza biashara ndogo, biashara za kati na kampuni changa ili kujijengea kipato katika Sekta za Mifugo na Uvuvi. Mikopo hiyo itatolewa kwa njia ya vifaa na pembejeo za uzalishaji, ikiwemo ufugaji wa samaki kwa vizimba, ufugaji wa kuku (chotara, mayai na nyama), mbuzi, kondoo na nguruwe, pamoja na boti za kuhudumia vizimba, boti za uvuvi, zana za uvuvi, mifumo ya ubari (cold chain) katika mazao ya uvuvi, mifumo ya kulazisha vifaranga vya samaki, mifumo na vifaa vya uchakataji wa mazao ya uvuvi ikijumuisha makausho ya dagaa na mwani (dryers). Vigezo na maelekezo kwa waombaji ni kama ifuatavyo: i. Baru...

NAFASI 200 ZA AJIRA ZA MAFUNDI ZATANGAZWA KWA KAZI NCHINI SAUDI ARABIA

  Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, kwa kushirikiana na Atilis Investment Limited , inawataarifu Watanzania wenye sifa stahiki kuhusu nafasi 200 za ajira za mafundi katika sekta ya ujenzi , zilizotolewa na kampuni ya Shade Corporation Limited ya nchini Saudi Arabia. KADA ZINAZOHITAJIKA Nafasi hizo zinahusisha mafundi wa kada mbalimbali, wakiwemo: Mafundi Uashi Mafundi Useremala Wasuka Nondo SIFA ZA MWOMBAJI Mwombaji anatakiwa kuwa na: Elimu ya astashahada kutoka chuo cha ufundi kinachotambuliwa na Serikali; Uzoefu wa kazi wa miaka miwili (2) au zaidi katika sekta ya ufundi; Uwezo na uzoefu katika kada husika, ikiwemo Uashi, Useremala au Usuka Nondo; Umri kati ya miaka 21 hadi 40 ; Waombaji wa nafasi hizi wanatakiwa kuwa wanaume . MASHARTI NA MAFANO YA AJIRA Waombaji watakaofaulu mchakato wa ajira watapata fursa ya kufanya kazi nchini Saudi Arabia kwa masharti yaliyowekwa na mwajiri. Miongoni mwa mafao na masharti ya ajira ni: Mshahara wa Riyal 1...

MHE. MBUNGE KANONI ASHIRIKI MAZISHI YA WAATHIRIKA WA AJALI KAZILA, ATOA WITO WA UPENDO, UMOJA NA MSHIKAMANO

  KALAMBO: Mbunge wa Jimbo la Kalambo, Mhe. Edefonsi Joackim Kanoni , ameshiriki mazishi ya wananchi wawili waliofariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea katika Kijiji cha Kazila, Kata ya Mwazye, Wilaya ya Kalambo, huku akitoa pole na faraja kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki pamoja na wananchi wote walioguswa na msiba huo. Ajali hiyo ilitokea tarehe 05 Agosti 2026 , wakati gari aina ya Fuso lililokuwa limebeba watu waliokuwa wakielekea kwenye shughuli ya harusi kutoka Kijiji cha Msoma, Kata ya Mwazye, Wilaya ya Kalambo , lilipofika katika Kijiji cha Kazila kwa ajili ya shughuli ya kufunga ndoa. Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa, gari hilo lilikuwa limembeba bwana harusi, Hosea Gilbert Watua , pamoja na watu wengine waliokuwa wakisafiri naye kutoka Kijiji cha Msoma kuelekea Kijiji cha Kazila, ambako alikuwa akienda kufunga ndoa na bibi harusi, Mehili Sauli Visent , mkazi wa Kijiji cha Kazila, Kata ya Mwazye. AJALI YATOKEA KABLA YA KUFIKA KWENYE DARAJA Taarifa zinaeleza ...