Kwa masikitiko makubwa, Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Kalambo, Mhe. Edefonsi Joackim Kanoni, inatoa salamu za pole kwa Mama yetu, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kufuatia kifo cha mume wake, Mzee Hafidh Ameir Hassan.
Katika kipindi hiki kigumu cha majonzi, Mhe. Mbunge pamoja na wananchi wa Jimbo la Kalambo tunaungana nawe, familia, ndugu, jamaa na marafiki katika kuomboleza msiba huu mkubwa.
Tunamuomba Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu Hafidh Ameir Hassan mahali pema peponi, na ampe Mama yetu Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na familia yote subira, faraja na nguvu katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo.
Pole sana Mama yetu Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Mungu ailaze roho ya Marehemu baba yetu Hafidh Ameir Hassan mahali pema peponi. Amina.
IMETOLEWA NA:
Musa Frackison Mzopola
Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Kalambo


💬 Toa Maoni Kuhusu Habari Hii
Umemaliza kusoma habari hii? Tupe maoni, mtazamo au swali lako hapa chini.
Comments
Post a Comment