📰 HABARI MPYA
Inapakia habari...

MBUNGE WA JIMBO LA KALAMBO MHE. EDIFONSI KANONI AENDELEA KUTEKELEZA AHADI YA UMEME KWA VITONGOJI VYOTE VYA JIMBO LA KALAMBO

MBUNGE WA JIMBO LA KALAMBO MHE. EDIFONSI KANONI AENDELEA KUTEKELEZA AHADI YA UMEME KWA VITONGOJI VYOTE VYA JIMBO LA KALAMBO

 


Mhe. Edifonsi Joackim Kanoni, Mbunge wa Jimbo la Kalambo, anaendelea ahadi aliyoitoa kwa wananchi wakati wa kampeni za uchaguzi kwa maamuzi na dira ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia Ilani ya Uchaguzi wa mwaka 2025–2030, ambayo inalenga kuwa na vitongoji vyote 422 vya Jimbo la Kalambo vinafikiwa na huduma ya umeme ifikapo mwaka 2030.

Katika miezi sita tangu aanze kutekeleza majukumu yake kama Mbunge wa Jimbo la Kalambo, Mhe. Kanoni ameendelea kupambania maendeleo ya wananchi wake kwa vitendo. Kupitia juhudi zake za karibu na Serikali pamoja na Wakala wa Nishati Vijijini (REA), vitongoji 35 tayari vimeidhinishwa kuunganishwa na huduma umeme ambapo mkataba umeshasainiwa, upembuzi yakinifu umekamilika na kazi ya kusambaza nguzo imeanza rasmi.

Hatua hii ni sehemu ya utekelezaji wa mpango mkubwa wa kusaidia wananchi wote wa Kalambo wanapata huduma ya umeme kwa ajili ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Kwa sasa vimebakia vitongoji 28 ili kukamilisha awamu ya utekelezaji.

Mhe. Kanoni amewaomba wananchi maeneo ambayo bado hayajafikiwa na huduma ya umeme kuwa na subira, akieleza miradi ya REA kutekeleza na mipango na upatikanaji wa rasilimali. Amesisitiza kuwa vitongoji vyote vilivyobaki vitafikiwa kwa mujibu wa ratiba ya Serikali.

Aidha, Mbunge huyo ameipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya uongozi wa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pamoja na Mawaziri, viongozi na watendaji mbalimbali wa Serikali kwa wanaompatia maendeleo yanafika kwa wananchi wa Kalambo na Watanzania kwa ujumla.

Amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuonesha kuwa ni serikali sikivu, inayojali na kuthamini maisha ya Watanzania kwa kupeleka huduma muhimu za maendeleo hadi ngazi ya wananchi wa kawaida.

Mhe. Kanoni amewasihi wananchi wa Kalambo kuendelea kuiamini Serikali yao, kuunga mkono juhudi za maendeleo zinazotekelezwa na umoja, mshikamano na utu, akisisitiza ndiyo msingi wa maendeleo.

Orodha ya Vitongoji Vilivyopangwa Kufikiwa na Umeme katika Awamu Hii

  1. Nchenje – Kijiji Utengule, Kata Mambwenkowe

  2. Mombokaku – Kijiji Mombo, Kata Legezamwendo

  3. Kawala – Kijiji Kanyalakata, Kata Mbuluma

  4. Uhuru – Kijiji Mlenje, Kata Legezamwendo

  5. Nchese – Kijiji Kachele, Kata Kisumba

  6. Kavusha – Kijiji Kileweli, Kata Kasanga

  7. Kantundulu – Kijiji Kalembe, Kata Mambwenkowe

  8. Molwe – Kijiji Muzi, Kata Kasanga

  9. Kalepa – Kijiji Kisala, Kata Samazi

  10. Mkwavi – Kijiji Kisala, Kata Samazi

  11. Namkonda – Kijiji Chipapa, Kata Mwimbi

  12. Mkombo – Kijiji Mkombo, Kata Legezamwendo

  13. Fena – Kijiji Kalepula “A”, Kata Ulumi

  14. Kasamvu – Kijiji Mikonko, Kata Matai

  15. Katindizi – Kijiji Mpombwe, Kata Mpombwe

  16. Iyala – Kijiji Chipapa, Kata Mwimbi

  17. Mizumbi – Kijiji Itekesha, Kata Kilesha

  18. Kamisuku – Kijiji Kanyezi, Kata Kanyezi

  19. Mchenje – Kijiji Kantalemwa, Kata Mnamba

  20. Chaptuka – Kijiji Kapozwa, Kata Mpombwe

  21. Mwela – Kijiji Safu, Kata Katete

  22. Mlembuke/Kapewa – Kijiji Sopa, Kata Sopa

  23. Wala – Kijiji Katazi, Kata Katazi

  24. Mipapa – Kijiji Msipazi, Kata Mnamba

  25. Makale – Kijiji Kaluko, Kata Katete

Vitongoji vinavyo Subiri Kuhidhinishwa na kuingia kwenye Mpango wa Utekelezaji

  1. Kamatwa – Kijiji Katuka, Kata Msanzi

  2. Munwa – Kijiji Limba, Kata Mkowe

  3. Kanamwene – Kijiji Mzungu, Kata Kalembe

  4. Lolesha – Kijiji Madibila, Kata Mambwenkowe

  5. Mbita – Kijiji Kipampa, Kata Samazi

  6. Isale – Kijiji Madibila, Kata Mambwenkowe

  7. Miakasi – Kijiji Kisala, Kata Samazi

  8. Mbangizya – Kijiji Mtutumbe, Kata Sopa

  9. Kalemasha – Kijiji Lolesha, Kata Mbuluma

  10. Kamisuku – Kijiji Mpanga, Kata Mambwenkowe

“Umoja, Mshikamano na Utu ndiyo nguzo ya maendeleo.”

KAZI NA UTU, TUNASONGA MBELE

Imetolewa na:
Musa Frackison Mzopola
Katibu wa Mbunge, Jimbo la Kalambo .


MATUKIO KWA NJIA YA PICHA

Inapakia picha...

HABARI MAARUFU

ZIARA YA MHE. KANONI KATIKA JIMBO LA KALAMBO IMEAIRISHWA; HIKI NDICHO KILICHOSABABISHA.

  Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Kalambo, Mhe. Edefonsi Joackim Kanoni , inapenda kuwataarifu wananchi wote wa Jimbo la Kalambo na umma kwa ujumla kuwa ziara iliyokuwa imepangwa kufanyika kuanzia tarehe 20 Julai 2026 hadi tarehe 10 Agosti 2026 imeahirishwa. Uamuzi huo umetokana na zuio la Serikali kuhusu kufanyika kwa mikutano ya hadhara katika kipindi hiki. Ofisi ya Mbunge inaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza na inaendelea kuwashukuru wananchi kwa ushirikiano na uelewa wao. Kwa taarifa zaidi na maendeleo ya shughuli za Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Kalambo, tembelea: www.mbungekalambo.com Imetolewa na: Musa Frackison Mzopola Katibu wa Mbunge, Jimbo la Kalambo

HATIMAYE! ORODHA RASMI YA WANUFAIKA WA MIKOPO YA WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI KWA WILAYA YA KALAMBO YATOLEWA – WANUFAIKA WOTE WATAKIWA KUHUDHURIA MAFUNZO MUHIMU

  TAARIFA KWA UMMA Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Kalambo, Mhe. Edefonsi Joackim Kanoni , inapenda kuwajulisha wananchi wote wa Wilaya ya Kalambo kuwa Wizara ya Mifugo na Uvuvi imekamilisha mapitio ya maombi ya mikopo yaliyowasilishwa na wananchi wa Wilaya ya Kalambo kupitia programu ya uwezeshaji wa wananchi kiuchumi. Kutokana na mchakato huo, Wizara imetoa rasmi orodha ya wanufaika waliokidhi vigezo na kufanikiwa kupata mikopo hiyo. Wanufaika kutoka Wilaya ya Kalambo ni kama ilivyoainishwa katika orodha rasmi ya Wizara, ambayo inajumuisha: Rahel John Mawela – Mradi wa Mbuzi Faustina Cladio Msumeno – Mradi wa Kuku wa Mayai William Isaya Moringe – Mradi wa Mbuzi Mashaka Medard Jastin – Mradi wa Mfumo wa Ubaridi Aibini Leonard John – Mradi wa Mbuzi Britney Shadi Pandisha – Mradi wa Kuku wa Nyama Sisilia Augustino Michael – Mradi wa Mbuzi Ofisi ya Mbunge inawapongeza wanufaika wote kwa kufanikiwa kupata fursa hiyo muhimu na inawatakia mafanikio katika utekelezaji wa ...

ZIARA YA MIKUTANO YA HADHARA YA MHE. EDEFONSI JOACKIM KANONI MBUNGE JIMBO LA KALAMBO YATANGAZWA

  Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Kalambo inapenda kuwataarifu wananchi wote wa Jimbo la Kalambo kuwa Mhe. Edefonsi Joackim Kanoni (Mb), Mbunge wa Jimbo la Kalambo, atafanya ziara ya mikutano ya hadhara katika kata na vijiji mbalimbali vya jimbo kuanzia tarehe 20 Julai, 2026 hadi tarehe 10 Agosti, 2026, kwa mujibu wa ratiba iliyoambatanishwa.    Ziara hii inalenga kuimarisha mawasiliano kati ya Mbunge na wananchi kwa kukutana nao ana kwa ana, kusikiliza maoni, kero na changamoto zinazowakabili, pamoja na kupokea mapendekezo yatakayosaidia kuboresha huduma za kijamii na kuharakisha maendeleo ya Jimbo la Kalambo. Aidha, Mhe. Mbunge atatoa mrejesho kuhusu utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kueleza mipango ya maendeleo inayotarajiwa kutekelezwa katika maeneo mbalimbali ya jimbo. Wananchi watapata fursa ya kuuliza maswali, kutoa maoni yao na kushiriki katika kujadili masuala muhimu yanayohusu maendeleo ya kata na vijiji vyao. Ushiriki wa wananchi katika mikutano hii ni msingi m...