📰 HABARI MPYA
Inapakia habari...

MHE. EDIFONSI KANONI ATEULIWA KUWA MJUMBE WA CHAMA CHA KIRAFIKI KATI YA BUNGE LA TANZANIA NA BUNGE LA INDIA

MHE. EDIFONSI KANONI ATEULIWA KUWA MJUMBE WA CHAMA CHA KIRAFIKI KATI YA BUNGE LA TANZANIA NA BUNGE LA INDIA

 


Mbunge wa Jimbo la Kalambo, Mhe. Edifonsi Joackim Kanoni, ameteuliwa rasmi kuwa mmoja wa wajumbe 10 wanaounda Chama cha Kirafiki cha Kibunge kati ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Bunge la India.

Kwa mujibu wa barua ya Katibu wa Bunge yenye kumbukumbu namba QA.203/261/01/48 ya tarehe 15 Juni 2026, uteuzi huo umefanywa na Spika wa Bunge, Mhe. Mussa Azzan Zungu (Mb), kwa lengo la kuimarisha ushirikiano, urafiki na diplomasia ya kibunge kati ya Tanzania na India.

Chama hicho kinaundwa na wabunge 10 walioteuliwa kutoka Bunge la Tanzania kwa ajili ya kushiriki shughuli mbalimbali za kuendeleza mahusiano ya kirafiki na kubadilishana uzoefu katika sekta mbalimbali za maendeleo kati ya nchi hizo mbili.

Aidha, Balozi wa India nchini Tanzania anatarajiwa kukutana na kufanya mazungumzo na wajumbe wa chama hicho tarehe 24 au 25 Juni 2026 katika Ofisi za Bunge jijini Dodoma, ikiwa ni sehemu ya kuimarisha ushirikiano kati ya mabunge ya nchi hizo mbili.

Uteuzi wa Mhe. Kanoni ni heshima kubwa kwa Jimbo la Kalambo, Mkoa wa Rukwa na Taifa kwa ujumla, ukiwa ni ishara ya imani kubwa aliyopewa katika kuwakilisha Tanzania kwenye masuala ya ushirikiano wa kimataifa kupitia diplomasia ya kibunge.

Imetolewa

Musa Frackison Mzopola

Katibu wa Mbunge jimbo la Kalambo

MATUKIO KWA NJIA YA PICHA

Inapakia picha...

HABARI MAARUFU

ZIARA YA MHE. KANONI KATIKA JIMBO LA KALAMBO IMEAIRISHWA; HIKI NDICHO KILICHOSABABISHA.

  Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Kalambo, Mhe. Edefonsi Joackim Kanoni , inapenda kuwataarifu wananchi wote wa Jimbo la Kalambo na umma kwa ujumla kuwa ziara iliyokuwa imepangwa kufanyika kuanzia tarehe 20 Julai 2026 hadi tarehe 10 Agosti 2026 imeahirishwa. Uamuzi huo umetokana na zuio la Serikali kuhusu kufanyika kwa mikutano ya hadhara katika kipindi hiki. Ofisi ya Mbunge inaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza na inaendelea kuwashukuru wananchi kwa ushirikiano na uelewa wao. Kwa taarifa zaidi na maendeleo ya shughuli za Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Kalambo, tembelea: www.mbungekalambo.com Imetolewa na: Musa Frackison Mzopola Katibu wa Mbunge, Jimbo la Kalambo

HATIMAYE! ORODHA RASMI YA WANUFAIKA WA MIKOPO YA WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI KWA WILAYA YA KALAMBO YATOLEWA – WANUFAIKA WOTE WATAKIWA KUHUDHURIA MAFUNZO MUHIMU

  TAARIFA KWA UMMA Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Kalambo, Mhe. Edefonsi Joackim Kanoni , inapenda kuwajulisha wananchi wote wa Wilaya ya Kalambo kuwa Wizara ya Mifugo na Uvuvi imekamilisha mapitio ya maombi ya mikopo yaliyowasilishwa na wananchi wa Wilaya ya Kalambo kupitia programu ya uwezeshaji wa wananchi kiuchumi. Kutokana na mchakato huo, Wizara imetoa rasmi orodha ya wanufaika waliokidhi vigezo na kufanikiwa kupata mikopo hiyo. Wanufaika kutoka Wilaya ya Kalambo ni kama ilivyoainishwa katika orodha rasmi ya Wizara, ambayo inajumuisha: Rahel John Mawela – Mradi wa Mbuzi Faustina Cladio Msumeno – Mradi wa Kuku wa Mayai William Isaya Moringe – Mradi wa Mbuzi Mashaka Medard Jastin – Mradi wa Mfumo wa Ubaridi Aibini Leonard John – Mradi wa Mbuzi Britney Shadi Pandisha – Mradi wa Kuku wa Nyama Sisilia Augustino Michael – Mradi wa Mbuzi Ofisi ya Mbunge inawapongeza wanufaika wote kwa kufanikiwa kupata fursa hiyo muhimu na inawatakia mafanikio katika utekelezaji wa ...

ZIARA YA MIKUTANO YA HADHARA YA MHE. EDEFONSI JOACKIM KANONI MBUNGE JIMBO LA KALAMBO YATANGAZWA

  Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Kalambo inapenda kuwataarifu wananchi wote wa Jimbo la Kalambo kuwa Mhe. Edefonsi Joackim Kanoni (Mb), Mbunge wa Jimbo la Kalambo, atafanya ziara ya mikutano ya hadhara katika kata na vijiji mbalimbali vya jimbo kuanzia tarehe 20 Julai, 2026 hadi tarehe 10 Agosti, 2026, kwa mujibu wa ratiba iliyoambatanishwa.    Ziara hii inalenga kuimarisha mawasiliano kati ya Mbunge na wananchi kwa kukutana nao ana kwa ana, kusikiliza maoni, kero na changamoto zinazowakabili, pamoja na kupokea mapendekezo yatakayosaidia kuboresha huduma za kijamii na kuharakisha maendeleo ya Jimbo la Kalambo. Aidha, Mhe. Mbunge atatoa mrejesho kuhusu utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kueleza mipango ya maendeleo inayotarajiwa kutekelezwa katika maeneo mbalimbali ya jimbo. Wananchi watapata fursa ya kuuliza maswali, kutoa maoni yao na kushiriki katika kujadili masuala muhimu yanayohusu maendeleo ya kata na vijiji vyao. Ushiriki wa wananchi katika mikutano hii ni msingi m...