TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Kalambo: Mbunge wa Jimbo la Kalambo, Mhe. Edefonsi Joackim Kanoni, anatarajia kufanya ziara katika maeneo mbalimbali ya Jimbo la Kalambo kwa ajili ya kukutana na wananchi kupitia mikutano ya hadhara pamoja na shughuli nyingine zilizopangwa katika ratiba ya ziara hiyo.
Ziara hiyo inalenga kumpa Mhe. Mbunge fursa ya kusikiliza na kupokea maoni, kero na changamoto za wananchi, pamoja na kujadiliana nao kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu maendeleo ya Jimbo la Kalambo.
Aidha, katika mikutano hiyo, Mhe. Edefonsi Joackim Kanoni ataeleza utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi na hatua mbalimbali zilizofikiwa katika kipindi cha miezi tisa tangu alipoingia madarakani, pamoja na kueleza mipango na mambo yanayoendelea kufanyiwa kazi kwa ajili ya kuwaletea wananchi maendeleo.
Mhe. Mbunge pia atatumia ziara hiyo kuendelea kuimarisha mawasiliano na ushirikiano kati yake na wananchi, kufuatilia changamoto zinazowakabili wananchi katika maeneo mbalimbali na kusikiliza hoja zao kwa lengo la kuzifikisha katika mamlaka husika na kuzifanyia kazi.
Mikutano hiyo itakuwa fursa kwa wananchi kuuliza maswali, kutoa maoni na kuwasilisha hoja zao kuhusu masuala ya maendeleo, huduma za kijamii na changamoto nyingine zinazowakabili katika maeneo yao.
Wananchi wote katika maeneo yaliyopangwa wanakaribishwa kushiriki kwa wingi katika mikutano hiyo.
RATIBA YA ZIARA YA MHE. MBUNGE JIMBO LA KALAMBO
Na.| Tarehe| Kata| Kijiji/Mahali| Tukio| Muda
1| 20-09-2026| MKOWE| MKOWE| Harambee – Kanisa la RC| 07:00 mchana – 11:00 jioni
2| 21-09-2026| MNAMBA| MTULA| Mkutano wa hadhara| 04:00 asubuhi – 06:00 mchana
| 21-09-2026| MNAMBA| KANTALEMWA| Mkutano wa hadhara| 07:00 mchana – 09:00 alasiri
| 21-09-2026| MNAMBA| MSIPAZI| Mkutano wa hadhara| 10:00 jioni – 12:00 jioni
3| 22-09-2026| MAMBWEKENYA| MPANGA| Mkutano wa hadhara| 04:00 asubuhi – 06:00 mchana
| 22-09-2026| MAMBWEKENYA| KAZOZYA| Mkutano wa hadhara| 07:00 mchana – 09:00 alasiri
| 22-09-2026| MAMBWEKENYA| KIUNDI| Mkutano wa hadhara| 10:00 jioni – 12:00 jioni
4| 23-10-2026| LEGEZAMWENDO| MOMBO| Mkutano wa hadhara| 04:00 asubuhi – 06:00 mchana
| 23-10-2026| LEGEZAMWENDO| MKOMBO| Mkutano wa hadhara| 07:00 mchana – 09:00 alasiri
| 23-10-2026| LEGEZAMWENDO| MLENJE| Mkutano wa hadhara| 10:00 jioni – 12:00 jioni
5| 24-10-2026| MAMBWENKOSWE| TUNYI| Mkutano wa hadhara| 04:00 asubuhi – 06:00 mchana
| 24-10-2026| MAMBWENKOSWE| MZUNGWA| Mkutano wa hadhara| 07:00 mchana – 09:00 alasiri
| 24-10-2026| MAMBWENKOSWE| KASUSU| Mkutano wa hadhara| 10:00 jioni – 12:00 jioni
6| 25-10-2026| MAMBWENKOSWE| UTENGULE| Mkutano wa hadhara| 04:00 asubuhi – 06:00 mchana
| 25-10-2026| MAMBWENKOSWE| ILONGA| Kikao cha ndani| 07:00 mchana – 09:00 alasiri
| 25-10-2026| MAMBWENKOSWE| ILONGA| Mkutano wa hadhara| 10:00 jioni – 12:00 jioni
7| 26-09-2026| LYOWA| MATAI B| Kikao cha ndani – Wawakilishi wa Bodaboda| 05:00 mchana – 08:00 mchana
| 26-09-2026| LYOWA| SANTAMARIA| Mkutano wa hadhara| 09:00 alasiri – 12:00 jioni
8| 27-09-2026| ULUMI| KALE| Mkutano wa hadhara| 04:00 asubuhi – 06:00 mchana
| 27-09-2026| MNAMBA| MNAZI| Mkutano wa hadhara| 07:00 mchana – 09:00 alasiri
| 27-09-2026| ULUMI| ULUMI| Mkutano wa hadhara| 10:00 jioni – 12:00 jioni
9| 28-09-2026| KASANGA| KANTALAMBA| Mkutano wa hadhara| 04:00 asubuhi – 06:00 mchana
| 28-09-2026| KASANGA| KASISI| Mkutano wa hadhara| 01:00 jioni – 08:00 jioni
| 28-09-2026| KASANGA| KAPELE| Mkutano wa hadhara| 09:00 mchana – 10:00 jioni
| 28-09-2026| KASANGA| KIPWA| Mkutano wa hadhara| 11:00 jioni – 12:00 jioni
10| 29-09-2026| KASANGA| MUZI| Mkutano wa hadhara| 04:00 asubuhi – 06:00 mchana
| 29-09-2026| KASANGA| KASANGA| Mkutano wa hadhara| 07:00 mchana – 09:00 alasiri
| 29-09-2026| KASANGA| KILEWANI| Mkutano wa hadhara| 10:00 jioni – 12:00 jioni
11| 30-09-2026| SAMAZI| KIPANGA| Mkutano wa hadhara| 04:00 asubuhi – 06:00 mchana
| 30-09-2026| SAMAZI| KATILI| Mkutano wa hadhara| 07:00 mchana – 09:00 alasiri
| 30-09-2026| SAMAZI| SAMAZI| Mkutano wa hadhara| 10:00 jioni – 12:00 jioni
12| 11-10-2026| LYOWA| MATAI B| Kufunga Ligi ya Wilaya| 08:00 mchana – 11:00 alasiri
Imetolewa na
Musa Frackison Mzopola
Katibu wa Mbunge Jimbo la Kalambo


💬 Toa Maoni Kuhusu Habari Hii
Umemaliza kusoma habari hii? Tupe maoni, mtazamo au swali lako hapa chini.
Comments
Post a Comment