📰 HABARI MPYA
Inapakia habari...

OFISI YA MBUNGE JIMBO LA KALAMBO YATOA WITO KWA VIKUNDI KUOMBA MIKOPO YA ASILIMIA 10

OFISI YA MBUNGE JIMBO LA KALAMBO YATOA WITO KWA VIKUNDI KUOMBA MIKOPO YA ASILIMIA 10

 

KALAMBO, TANZANIA — Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Kalambo, Mheshimiwa Edefonsi Joackim Kanoni, inapenda kuwataarifu wananchi wote wa Jimbo la Kalambo kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo ametangaza mikopo ya asilimia 10 yenye thamani ya shilingi milioni mia tatu (TSh 300,000,000) kwa ajili ya vikundi vya vijana wenye umri wa miaka 18 hadi 45, wanawake na watu wenye ulemavu.

Mikopo hiyo inalenga kuwawezesha wanufaika kuimarisha shughuli zao za kiuchumi, kuendeleza miradi waliyoianzisha na kuongeza fursa za kujikwamua kiuchumi.

MASHARTI YA UOMBAJI WA MIKOPO

Ili kikundi kiweze kuomba mkopo huo, kinapaswa kutimiza masharti yafuatayo:

  1. Usajili wa kikundi: Kikundi kiwe kimesajiliwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo.

  2. Mradi ulioanzishwa: Kikundi kiwe tayari kimeanzisha mradi unaokusudiwa kuendelezwa kupitia mkopo huo.

  3. Barua ya maombi: Kikundi kiandike barua ya maombi ya mkopo na kuiwasilisha kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo, S.L.P. 3, Matai-Kalambo.

  4. Muhtasari wa kikao: Barua ya maombi iambatane na muhtasari wa kikao cha kikundi unaoonesha makubaliano ya wanakikundi ya kuomba mkopo.

  5. Mchanganuo wa mradi: Kikundi kiambatishe mchanganuo unaoonesha namna fedha za mkopo zitakavyotumika kuendeleza mradi husika.

TAREHE YA MWISHO YA KUWASILISHA MAOMBI

Ofisi ya Mbunge inavikumbusha vikundi vyote vinavyokidhi vigezo kuandaa nyaraka zinazohitajika na kuwasilisha maombi yao kwa wakati, kwa kuzingatia kuwa tarehe ya mwisho ya kuwasilisha maombi ni Oktoba 30, 2026.

Wananchi, hususan vijana, wanawake na watu wenye ulemavu, wanahimizwa kutumia fursa hii ya mikopo kuendeleza miradi yao, kukuza shughuli za uzalishaji na kuimarisha hali zao za kiuchumi.

Imetolewa na:

Musa Frackison Mzopola
Katibu wa Mbunge, Jimbo la Kalambo


Umemaliza kusoma habari hii? Tupe maoni, mtazamo au swali lako hapa chini.

Comments

MATUKIO KWA NJIA YA PICHA

Inapakia picha...

HABARI MAARUFU

FURSA ZA MIKOPO YA VIJANA SASA HADHARANI OMBA SASA UJIKWAMUE KIUCHUMI

  Katika kutekeleza ahadi ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya kutoa shilingi bilioni 200 kwa vijana ndani ya siku 100 baada ya kuingia madarakani, Wizara ya Mifugo na Uvuvi inautangazia umma kuanza kwa Awamu ya Pili ya utoaji wa mikopo yenye masharti nafuu kwa vijana. Malengo ya mikopo hiyo ni kuwawezesha vijana kupata mitaji ya kuanzisha na kuendeleza biashara ndogo, biashara za kati na kampuni changa ili kujijengea kipato katika Sekta za Mifugo na Uvuvi. Mikopo hiyo itatolewa kwa njia ya vifaa na pembejeo za uzalishaji, ikiwemo ufugaji wa samaki kwa vizimba, ufugaji wa kuku (chotara, mayai na nyama), mbuzi, kondoo na nguruwe, pamoja na boti za kuhudumia vizimba, boti za uvuvi, zana za uvuvi, mifumo ya ubari (cold chain) katika mazao ya uvuvi, mifumo ya kulazisha vifaranga vya samaki, mifumo na vifaa vya uchakataji wa mazao ya uvuvi ikijumuisha makausho ya dagaa na mwani (dryers). Vigezo na maelekezo kwa waombaji ni kama ifuatavyo: i. Baru...

NAFASI 200 ZA AJIRA ZA MAFUNDI ZATANGAZWA KWA KAZI NCHINI SAUDI ARABIA

  Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, kwa kushirikiana na Atilis Investment Limited , inawataarifu Watanzania wenye sifa stahiki kuhusu nafasi 200 za ajira za mafundi katika sekta ya ujenzi , zilizotolewa na kampuni ya Shade Corporation Limited ya nchini Saudi Arabia. KADA ZINAZOHITAJIKA Nafasi hizo zinahusisha mafundi wa kada mbalimbali, wakiwemo: Mafundi Uashi Mafundi Useremala Wasuka Nondo SIFA ZA MWOMBAJI Mwombaji anatakiwa kuwa na: Elimu ya astashahada kutoka chuo cha ufundi kinachotambuliwa na Serikali; Uzoefu wa kazi wa miaka miwili (2) au zaidi katika sekta ya ufundi; Uwezo na uzoefu katika kada husika, ikiwemo Uashi, Useremala au Usuka Nondo; Umri kati ya miaka 21 hadi 40 ; Waombaji wa nafasi hizi wanatakiwa kuwa wanaume . MASHARTI NA MAFANO YA AJIRA Waombaji watakaofaulu mchakato wa ajira watapata fursa ya kufanya kazi nchini Saudi Arabia kwa masharti yaliyowekwa na mwajiri. Miongoni mwa mafao na masharti ya ajira ni: Mshahara wa Riyal 1...

MACHIFU KALAMBO WAMPA MHE. KANONI BARAKA NA KUMUHIMIZA KUENDELEA NA KAZI ZA MAENDELEO

  Mhe. Edefonsi Joackim Kanoni, Mbunge wa Jimbo la Kalambo, amekutana na kufanya kikao na Machifu wa Wilaya ya Kalambo, ambapo pamoja na mambo mengine, amewashukuru Machifu hao kwa baraka, ushauri na ushirikiano wao, pamoja na mchango wao katika safari yake ya kuingia katika nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Kalambo. Akizungumza katika kikao hicho, Mhe. Kanoni amewashukuru Machifu kwa kuendelea kutambua na kuunga mkono juhudi za maendeleo katika Jimbo la Kalambo, huku pia akiwashukuru wananchi wote walioshiriki katika kufanikisha ushindi wake. Aeleza utekelezaji wa Ilani ndani ya miezi tisa Mhe. Kanoni ameeleza mambo mbalimbali ya utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi yaliyofanyika katika kipindi cha miezi tisa tangu alipoingia madarakani, akieleza hatua mbalimbali zilizochukuliwa katika kushughulikia changamoto na mahitaji ya wananchi wa Kalambo. Ameomba Machifu pamoja na wananchi wote wa Kalambo kuendelea kushirikiana na kushikamana, akisisitiza kuwa umoja na mshikamano ni muhim...