Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, imetoa jumla ya shilingi bilioni 1.2 kwa ajili ya kulipa fidia kwa wananchi wa eneo la Tatanda Kasesya, Wilaya ya Kalambo, kufuatia ombi lililowasilishwa na Mbunge wa Jimbo la Kalambo, Mhe. Edefonsi Joackim Kanoni, kupitia Wizara husika na Bungeni.
Hatua hiyo ni utekelezaji wa ombi la muda mrefu la wananchi wa eneo hilo waliokuwa wakisubiri suluhisho la suala la fidia, ambalo limekuwa changamoto kwao kwa kipindi kirefu.
Fedha hizo tayari zimewasili, huku taratibu za kiutawala na malipo zikiendelea kukamilishwa ili wananchi husika waanze kupokea fidia zao.
Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Kalambo, chini ya Mhe. Edefonsi Joackim Kanoni, imetoa shukrani za dhati kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, mawaziri na watendaji wote wa Serikali kwa ushirikiano wanaoendelea kutoa katika kutatua changamoto zinazowakabili wananchi wa Kalambo.
Aidha, Ofisi ya Mbunge imewataka wananchi kuendelea kuiamini Serikali ya Awamu ya Sita, ikieleza kuwa ni Serikali sikivu inayojali, kusikiliza na kuthamini maisha na ustawi wa Watanzania.
Vilevile, wananchi wametakiwa kuendelea kutoa ushirikiano kwa Mbunge, madiwani na watendaji wote wa Serikali katika Jimbo la Kalambo, huku wakihimizwa kudumisha upendo, mshikamano na amani kwa ajili ya kuleta maendeleo ya jimbo hilo.
KAZI NA UTU TUNASONGA MBELE.
Imetolewa na:
Musa Frackison Mzopola
Katibu wa Mbunge
Jimbo la Kalambo.


💬 Toa Maoni Kuhusu Habari Hii
Umemaliza kusoma habari hii? Tupe maoni, mtazamo au swali lako hapa chini.
Comments
Post a Comment