Husika na mada tajwa hapo juu.
2\. Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Kalambo inawatangazia Vijana wote wa Wilaya ya Kalambo wanaopenda kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa utaratibu wa hiari kwa Mwaka 2026/2027 kujitokeza na kuomba nafasi hiyo.
3\. Utaratibu wa Maombi hayo unaratibiwa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya kwa kushirikiana na Ofisi ya Mshauri wa Jeshi la Akiba Wilaya ya Kalambo.
4\. ZINGATIA:
\- Maombi yataanza kupokelewa tarehe 13/11/2026 saa 1:30 Asubuhi mpaka 17/11/2026 saa 9:30 Alasiri na Usaili utafanyika tarehe 19/11/2026 kuanzia saa 01:00 asubuhi katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kalambo na siku hiyo Kila aliyeomba afike na vyeti halisi
\- Barua za maombi zitakazoandikwa zipitishwe kwa Watendaji wa Vijiji na Kata ili zisainiwe na kuwekwa muhuri.
5\. Aidha, maombi yote yawasilishwe katika Anuani hii:-
Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, 9 Barabara ya Mkurugenzi Mtendaji, S. L. P 1, MATAI, 55481 KALAMBO.
SIFA ZA KUZINGATIA
A. Awe raia wa Tanzania.
B. Umri na Elimu
1\. Kwa Vijana wenye Elimu ya Darasa la Saba umri ni kuanzia miaka 16 hadi 18, waliomaliza Elimu ya Msingi kuanzia mwaka 2023, 2024, 2025, na 2026 na awe na Cheti halisi cha kumaliza Elimu ya Msingi.
2\. Vijana wenye Elimu ya Kidato cha Nne umri usiwe zaidi ya miaka 20, waliomaliza Elimu ya Sekondari kuanzia mwaka 2022, 2023, 2024 na 2025. Awe na ufaulu wa daraja la kwanza hadi la nne. Aidha, Kijana mwenye ufaulu wa daraja la nne awe na alama kuanzia 26 hadi 32. Awe na Cheti halisi cha kumaliza Elimu ya Sekondari (Secondary Leaving Certificate) na Cheti halisi cha matokeo (Academic Certificate). Pamoja na cheti halisi cha kumaliza elimu ya msingi.
3\. Vijana wenye Elimu ya Kidato cha Sita umri usiwe zaidi ya miaka 22, waliomaliza Elimu ya Sekondari kuanzia mwaka 2022, 2023, 2024 na 2025. Awe na ufaulu wa daraja la kwanza hadi daraja la nne. Awe na Cheti halisi cha kumaliza Elimu ya Sekondari (Secondary Leaving Certificate) na Cheti halisi cha matokeo (Academic Certificate). Pamoja na cheti cha kumaliza elimu ya msingi.
4\. Vijana wenye Elimu ya Stashahada umri usiwe zaidi ya miaka 25. Aidha, awe na Vyeti halisi vya elimu ya msingi, elimu ya Sekondari pamoja na Chuo (cheti au hati ya matokeo).
5\. Vijana wenye elimu ya Shahada umri usiwe zaidi ya miaka 26, awe na vyeti halisi vya elimu ya msingi, elimu ya Sekondari pamoja na Chuo (cheti au hati ya matokeo).
6\. Vijana wenye Elimu ya Shahada ya Uzamili umri usiwe zaidi ya miaka 27. Aidha, Awe na Vyeti halisi vya elimu ya msingi, elimu ya Sekondari pamoja na Chuo (cheti au hati ya matokeo).
C. Awe na afya njema, Akili timamu na asiwe na alama yoyote ya michoro mwilini (Tattoo).
D. Mwenye tabia na nidhamu nzuri, hajapatikana na hatia Mahakamani na hajawahi kufungwa.
E. Awe na Kitambulisho cha Taifa au namba ya kitambulisho kutoka Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).
F. Awe na cheti halisi cha kuzaliwa (Original Birth Certificate).
G. Asiwe ametumikia Jeshi la Polisi, Magereza, Chuo cha Mafunzo au Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo wala kuajiriwa na Idara nyingine Serikalini.
H. Asiwe amepitia Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Operesheni za nyuma kwa kundi la kujitolea na kundi la lazima (Mujibu wa Sheria).
I. Asiwe anajihusisha/amejihusisha na matumizi ya madawa ya kulevya, bangi na mengine yanayofanana na hayo.
J. ANGALIZO: Kijana atakayepatikana na nyaraka za kughushi atachukuliwa hatua kali za kisheria kulingana na taratibu zilizopo.
Imetolewa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kalambo.
OFISI YA MBUNGE JIMBO LA KALAMBO
Ofisi ya Mbunge Jimbo la Kalambo, Mhe. Edefonsi Joackim Kanoni, inatoa wito kwa Wanakalambo wenye kukidhi vigezo waweze kuchangamkia fursa hiyo na kutuma maombi kwa wakati.


💬 Toa Maoni Kuhusu Habari Hii
Umemaliza kusoma habari hii? Tupe maoni, mtazamo au swali lako hapa chini.
Comments
Post a Comment